Breaking News

Waombolezaji wafanya mauaji ya Kikatili Katavi

POLISI mkoani Katavi  linawasaka watu wanaodaiwa  kumuua kikatili mkazi wa  kijiji cha Kapalala wilayani Mlele ,Rehema Msole(32)  kwa  kupigwa  na shoka  mawe  na nondo  na kisha mwili wake kuchomwa moto  wakimtuhumu kuwa mchawi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hilo  lilitokea kijijni hapo ,Septemba 13 saa 12  jioni baada la kundi la waombolezaji kumvamia  na kumshambulia kwa kumkata kwa shoka na kumpiga na nondo mawe fimbo na kisha waliuchoma mwili wake moto

Kidavashari alidai kuwa siku  chache  kabla ya tukio hilo  kulitokea  msiba kijijini hapo  nyumbani kwa  Christopher Baharia  ambaye alifiwa  na mtoto wake  aitwaye  Elizabeth Baharia

Alifafanua baaada ya kutokea kwa msiba huo  kuliibuka  hisia  kuwa kuna mtu  amemloga  binti huyo wakimshuku  Rehema  Msole

‘’Inasadikiwa   siku za  nyuma  wakati  ndugu wa marehemu  Elizabeth walipokuwa wakimuuguza   walimuona  Rehema  akichugulia  dirishani  katika chumba  alichokuwa amelala  mgonjwa huyo  kabla ya kufikwa na umauti .........Hivyo  ndugu hao walihisi kuwa mtu huyo aliyechungulia dirishani ni mchawi wao ‘’ alidai  Kamanda Kidavashari

Aliongeza kuwa  siku moja baada ya Elizabeth  kufariki, Rehema akiwa  na familia yake  nyumbani kwa Isaya  Kyejo aliona kundi waombolezaji  wakitokea kwenye msibani nyumbani kwa Christopher Baharia  ambao walizingira nyumba hiyo huku wakishauriana kilicho kuwa kimewaleta ndipo walipomvamia marehemu  na kuanza kumpiga kwa nondo shoka mawe na fombo  na kisha mwili wake kuuchoma moto huku wakidai kuwa marehemu ni mchawi

 Kamanda huyo alisema polisi linaendelea na uchunguzi wa  tukio hilo ambapo hadi sasa hakuna watu wala mtu aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo.

No comments