Breaking News

MAUAJI, WAWILI WAFA KATAVI KWA MATUKIO TOFAUTI

Na Walter Mguluchuma, 
Katavi.

WATU wawili wamefariki dunia mkoani Katavi katika matukio tofauti likiwemo mwanamke mmoja kujinyonga kwa kutumia kitenge chake kwa kile kilichoelezwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri  Kidavashari aliwaambia  waandishi wa  habari kuwa mwanamke huyo aliyejinyonga    hadi kufa alifahamika kwa jina la Milembe Charles (25)  Mkazi wa Kitongoji  cha Mtisi




 Alisema tukio la mwanamke  huyo kujinyonga  lilitokea  hapo  jana   saa kumi na mbili   jioni  katika shamba la wazazi wake lililopo kijini hapo
 Alifafanua kuwa  kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akiishi nyumbani kwa wazazi wake baada ya kuwa wametengana  na mume wake  ambaye walikuwa  na ugomvi nae kufuatia mume wa marehemu kuwa na mke mwingine kwenye Kijiji cha Kasekese  kitendo ambacho marehemu hakuwa ameridhishwa nacho
 Siku hiyo ya tukio marehemu  alikuwa  alikuwa  nyumbani kwa wazazi wake ndipo ilipofikia mida hiyo ya tukio aliondoka nyumbani kwa wazazi wake pasipo kuwa amewaaga kuwa anakwenda wapi
 Alisema wazazi wa marehemu  baada ya kuona muda umekuwa mrefu  tokea marehemu alipoondoka nyumbani walipata mashaka  na ndipo walipoamua kwenda nyumbani kwa mume wake kumtafuta hata hivyo mume wa marehemu aliwajibu kuwa siku hiyo alikuwa haja fika nyumbani kwake  

Jitihada za kumtafuta  ndipo zilianza na ndipo waliweza kumkuta marehemu akiwa amejinyonga hadi kufa  juu ya mti  wa mwembe  kwa kutumia kitenge chake  katika  kichaka kilichopo jirani na nyumba  ya wazazi wake


Katika tukio jingine, kijana  Shija  Ngasa (35) Mkazi wa Kijiji cha  Katuma Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameuwawa kikatili  kuchinjwa shingo  hadi kufa na watu wasio julikana  wakati akiwa na familia yake nymbani kwake wakisubilia  kula chakula cha jioni


Mauaji hayo ya kutisha  yalitokea  juzi  saa mbili   usiku nyumbani kwa marehemu  Shija   Ngasa katika Kijiji cha Katuma ambapo marehemu alikuwa akiishi na familia yake


Kamandahuyo alisema  kuwa  wakati wakiwa wanasubilia chakula  hicho ghafla walitokea watu wawili wasio fahamika  huku wakiwa  wamefunika uso wao  na mmoja wa watu hao alikuwa ameshika shoka mkononi


kisha watu hao walimvamia  marehemu  na  kuanza kumchinja kwa shoka  huku watoto wake  wawili wakiwa wanashuhudia  kitendo hicho cha mauaji
hayo.

Kidavashari  alisema  watoto   hao wa marehemu waliendelea kupiga mayowe ya  kuomba msaada kwa majirani  na  ambao walifika kwenye eneo  hilo na kukuta watu hao wameisha tokomea  kusiko fahamika huku mwili wa marehemu ukiwa unagalagala  chini


Chanzo cha mauaji   hayo ya kikatili   bado hakijajulikana na mpaka sasa hakuna  mtu  wala watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo


Kamanda huyo aliongeza kuwa  tukio la kwanza imebainika ni wivu wa mapenzi, lakini tukio jingine bado uchunguzi unaendelea na watuhumiwa wakitafutwa ili sheria ichukue mkondo wake.

No comments