Breaking News

WASWIDENI WAWATUNUKU TUZO WAANDISHI RUKWA.

Na Mwandishi wetu,
Sumbawanga.

WAANDISHI wa habari watano wa mkoa wa Rukwa, wakiongozwa na Mhariri wa blog ya Pembezonikabisa
wametunukiwa tuzo kwa kuwa na mchango mkubwa katika kuandika na kutangaza habari za afya na ujinsia.
Mhariri wa blog ya Pembezonikabisa, Mussa Mwangoka akipokea tuzo yake.
Waandishi hao wa habari ni Mussa Mwangoka ambaye licha ya kuwa mhariri wa mtandao huu pia ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Peti Siyame (Habarileo/Daily News), Joshua Joel (ITV), Nswima Ernest (TBC) na Juddy Ngonyanya kutoka Channel ten.
Mratibu msaidizi Shirika la Afya ya Uzazi la Sweden (RFSU), Eugenia Msasanuri, alisema kuwa waandishi hao wa habari walikuwa mstari wa mbele kuandika na kutangaza habari za Afya na Ujinsia kupitia mradi wa wa  ushirikishwaji wanaume Tanzania katika haki ya uzazi, afya na ujinsia(TMEP) ulikuwa ukitekelezwa katika mikoa miwili hapa nchini ya Rukwa na Singida.
Waandishi wakiwa wameshika tuzo walizotunukiwa na RFSU, hapo katika picha ya Pamoja na mlezi wa klabu ya waandishi ya Rukwa, Mkuu wa wilaya ya Nkasi Iddy Kimanta aliyeketi katikati.
Alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo, RFSU ilikuwa ikishirikiana na shirikali lisilo la kiserikali la Resource Oriented Development Initiative (RODI) kwa Rukwa na Health Action Promotion Association (HAPA) kwa upande wa Singida.
 
Tuzo hizo zilikwenda sambamba na kukabidhiwa vyeti ikiwa ni ishara ya kutambua na kuthamini mchango wao katika kuripoti taarifa hizo lengo likiwa ni la kuleta ushiriki sawa wanaume kwenye afya ya uzazi ambapo imesaidia kuhamasisha wanaume kuambatana na wake zao kliniki kabla, wakati na baada ya kujifingua lakini pia kufanya kuwepo na ushiriki wa moja kwa moja katika masuala ya uzazi na malezi ya familia.
 
Mwakilishi wa kituo cha Luninga cha ITV mkoa wa Rukwa,Joshua Joel akipokea tuzo yake.
Akikabidhi zawadi hizo, Afisa tawala wa mkoa wa Rukwa, Erasmus Rugarabamu baada ya kukabidhi tuzo hizo, aliwapongeza waandishi hao wa habari na kuongeza kuwa kuondoka kwa wafadhili kusiwe sababu ya kufa kwa mradi huo halmashauri husika zinapaswa kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu kwa manufaa ya jamii.
 
 Kwaupande wake, Peti Siyame ambaye pia Mwenyekiti wa Klabu wa waandishi wa habari ya Rukwa, alisema waandishi hao wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na weledi na sio tuzo walipata ziwafanye wabweteke na kusahau majukumu yao mbele ya jamii.



No comments