Breaking News

Singida United yalamba mamilioni ya SportPesa

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (kulia) akiwa na viongozi wa Singida United leo baada ya kusaini mkataba

Kampuni ya SportPesa leo imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na klabu ya Singida United kwa dau la Sh. Milioni 250.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema kwamba wameingia mkataba na timu hiyo kwa sababu imeonyesha nia ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao kutokana na usajili mzuri wanaoufanya.

“Tumeingia mkataba na Singida United ambayo ndiyo timu ya mwisho katika udhamini wa SportPesa nchini, kutokana na timu hii kuwa na maandalizi mazuri,”alisema Tarimba.
Tarimba alisema kwamba mkataba huo una kipengele cha kuongezwa iwapo Singida United itafanikiwa kubaki Ligi Kuu baada ya msimu ujao.
Mchezaji wa Singida United, Nizar Khalfan akiwa na jezi yenye nembo ya SportPesa

Kwa upande wake, kocha wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm alisema kwamba udhamini huo ni chachuya timu kufanya vizuri msimu ujao.

“Nafurahi baada ya mafanikio yangu nikiwa na Yanga, sasa Napata fursa nyingine nzuri ya kuendeleza mafanikio hayo na Singida United,”alisema.

Source: Bin Zubeiry sports online

No comments