KIDUCHU WAJITOKEZA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA MPANDA.
Na Mwandishi wetu, Katavi.
IMEELEZWA kuwa kutoahamasishwa kwa wananchi wa wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi ni miongoni mwa sababu zilizochangiwa kuwapo kwa idadi ndogo ya watu wanaojitokeza kutoa maoni ya kwenye tume ya kupokea maoni ya katiba mpya, imefahamika.
Mwenyekiti wa kamati ya kukusanya maoni ya Katiba mpya iliyopo mkoani humo hivi sasa, Mohamed Yusuph Mshamba alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Lyambalyamfipa mjini mpanda,
Ambapo kamati hiyo yenye wajumbe wa nne ilipokuwa ikitoa taarifa ya majumuisho ya mikutano yao waliofanya katika wilaya ya Mpanda.
Alisema kuwa changamoto kubwa waliokutana nayo ni kuwapo kwa mahudhurio kidogo ya watu katika wilaya hiyo hali ambayo ilitokana na hamasa ndogo hivyo watu wengi kutokuwa na mwamko wa kutoa maoni.
Mashamba alisema kuwa walishangazwa na mahudhurio ya wananchi wa kata ya Mishamo ambapo kwenye mkutano wao kulikuwa na watu wanne tu, huku kata ya Ikola ikiongozwa kwa idadi kuwa ya watu kujitokeza ambapo ilifikia 400.
Licha idadi ndogo ya watu, changamoto nyingine ni kutojitokeza kwa wanawake kwenye mikutano ya kupokea maoni ya marekebisho ya katiba na hao wachache wanao jitokeza wamekuwa hawachangii maoni yao.
Alisema pamoja na uchache wa watu kwenye mikutano hiyo wameweza kupata maoni mazuri ambayo yatasaidia kutengeneza katiba.
Nae mratibu wa tume hiyo Haji Omary haji aliwaomba wanasiasa na viqngozi wa tasisi mbalimbali waache tabia ya kutuma watu wapeleke maoni yao na badala yake wajitokeze wao wenyewe.
Wajumbe wa tume hiyo wamemaliza kukusanya maoni ya katiba mpya katika wilaya ya Mpanda na juzi walifanya mkutano wa wa kwanza wilayani mlele kwenye kata ya kasokola tarafa ya Nsimbo.
Mkuu wa mkoa wa Katavi, Rajabu Rutengwe. |

No comments