Breaking News

RC Rukwa awafunda Madiwani

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven Zelothe amewataka madiwani wa halmashauri za wilaya na Manispaa mkoani humo, kuhakikisha halmashauri zao zinatumia mashine za kieletroniki ili zitumike kukusanyia mapato na kuondokana na upotevu wake. 

Alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha kazi cha Madiwani kinacholenga kuboresha mfumo ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kupitia hamasa ya madiwani, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo. 

facebook.comAlisema kuwa licha ya jitihada za serikali kuu kuelekeza nguvu zake katika ukusanyaji mapato na kudhibiti upotevu wake lakini bado halmashauri za mkoa huo kuna mianya ya upotevu wa mapato hayo kwa Kuwa hazitumii machine za kieletroniko katika ukusanyaji huo.
                               Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Rukwa.

Zelothe alisema kuwa dalili za halmashauri kupoteza mapato yake zinajionyesha kutokana na halmashauri hizo kununua mashine 140 tu wakati mahitaji ni 438 hivyo ni dhairi kwamba bado kuna upotevu mkubwa wa mapato hayo.

Alitaka madiwani kuhakikisha halmashauri zinanunua mashine hizo na kuhakikisha zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa ili mapato yatakayopatika yatumike kuboresha huduma za kijamii. 
                                    Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa  ya Sumbawanga, Rukwa.

Naye,  Katibu tawala wa mkoa huo,  Tixon Nzunda alisema kwamba madiwani wana wajibu kuhakikisha kwamba halmashauri zao zinatumia mashine hizo kukusanya mapato katika kila sekta ikiwemo ya afya kupitia katika vituo vinavyotoa huduma hiyo ili fedha zitakazopatikana zitumike kuboresha huduma hizo.

Alisema lazima mashine hizo zinunuliwe ndani ya mwezi huu na kuanza kutumika mara moja  na iwapo itabaini bado kuna watendaji wa halmashauri wanaendelea kukusanya mapato kwa njia stakabadhi hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa Kuwa huo ni wizi wa mapato ya serikali na haukubaliki. 

Mkoa huo kupitia halmashauri zake ulikadiria kukusanya kupitia vyanzo vyake vya ndani kiasi cha Sh bilioni 9.2 lakini hadi sasa makusanyo yake ni asilimia 53.6 tu. 

No comments