Shughuli za kiuchumi zachangia kuharibu mazingira ya Rukwa na Katavi.
Ongezeko kubwa la shughuli za kiuchumi katika mikoa ya Rukwa na Katavi, inatajwa ni moja ya changomoto kubwa katika uhifadhi na usmamizi wa mazingira katika mikoa hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira ) Januari Makamba, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira ) , Mhandisi Ngosi Mwihava alisem,a hayo jana wakati wa uzinduzi wa mradi wa Jumuiko la Pamoja , Suluhisho la Pamoja (JUPASUPA) ulifanyika mjini hapa.
Mradi huo ni ushirikiano kati ya Serikali ya Uholanzi , Shirika la Kimatiaifa la Uhifadhi wa mazingira la Uholanzi (WWF NL) , Shirika la Kimataifa Kaengesa Rukwa (KAESO).
Alisema kutokana na mikoa hiyo kuwa na fursa nyingi za kiuchumi, kasi ya ongezeko la watu wanaofanya shughuli hizo imekuwa kubwa hasa katika maeneo ya Kilimo, ufugaji, Uvuvi, uchimbaji wa Madini, uboreshaji wa miundombinu na uwekezaji mkubwa hali ambayo inahitaji uangalifu wa ziada katika kuhifadhi na usimamizi wa mazingira.
Alisema uangalifu wa ziada unahitaji kwa kuwa watu na mifugo ambayo wote wanategemea mifumo ikilojia.
Alisema hali ya uharibu wa mazingira ni kubwa ambapo kil mtanzania hutumia takribani meta moja ya ujazo ya kuni au magogo kwa ajili ya nishati tu ikiwa ni sawa na zaidi ya meta za ujazo milioni 50 kwa mwaka.
Aidha kasi ya uangamizaji misitu nchini inakadiriwa kufikia ekari 372 , 000 kwa mwaka .
Mtendaji Mkuu wa KAESO , Ozem Chapita alisema kuwa mradi huo utatekelezwa katika mikoa miwili ya Rukwa na Katavi lengo likiwa kuhakikisha kunakuwa na usimamizi endelevu wa vyanzo vya maji , uhifadhi wa maliasili, uwekezaji rafiki wa mazingira na kuongeza jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ili kuhakikisha uendelevu wa mradi huu hasa katika utekelezaji katika ngazi ya Taifa asasi zingine zikiwemo Haki Ardhi , Action Aid Tanzania (AATZ) na Shirikisho la timu ya Wanasheria wa Mazingira Tanzania (LEAT) zitashiriki katika mradi huu kwa kusaidiana na Serikali katika kuandaa na kutekeleza sera bora na mipango madhubuti ya usimamizi wa ardhi , maliasili na hifadhi ya mazingira katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Rukwa , Albinus Mgonya alizitaka halmashauri zote za mikoa hiyo utendaj wake uwe na lengo la kutoa matokeo bora zaidi ili kunusuru rasilimali aslilia ili kuinusuru jamii ili kufanikisha mradi huo.
No comments