Breaking News

Manji ajiondoa rasmi Yanga.



Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusufali Manji amejiuzulu nafasi hiyo mapema leo. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii imeonyesha barua iliyosainiwa na Yusuf Mehbub Manji Mei 22 mwaka huu (yaani jana).

Taarifa hiyo imesema Manji ameamua kujiuzulu ili kutoa nafasi kwa wengine kuongoza klabu hiyo. Aidha hofu ya taarifa hiyo imezua masuala mengi na mijadala katika mitandao ya kijamii kuwa ni ya kweli au la. 
Kwa upande mwingine taarifa za ndani kutoka chanzo chetu zimetujuza kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo Charles Mkwasa amekubaliana na maombi ya Mwenyekiti huyo kujiuzulu.

Soma taarifa ya kujiuzulu kwa Manji.

“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Huwa kunafika muda tukiwa tunafuata wito Fulani, wakati mimi nikiwa sehemu ya YANGA ilinibidi nijitokeze mbele kwa ajili ya umoja wa Klabu yetu tuipendayo na kuongoza. Kulikuwa na Wanachama waliokuwa wakigombana, ndipo ulikuwa muda wangu wa kutoa msaada kwa YANGA.

Sikuweza kuendelea kujifanya kuwa siku hadi siku, kuwa atatokea mtu, sehemu Fulani na kuleta mabadiliko. Sisi sote ni sehemu ya ukoo mkubwa wa YANGA na ukweli mnaufahamu, imani ndiyo jambo ambalo tulihitaji ndani ya Yanga kuturudisha katika mwelekeo sahihi miaka 11 iliyopita.

Sasa hivi katika ulimwengu wa YANGA kama Mwenyekiti wa Klabu (heshima kubwa nitakayoienzi moyoni mwanguni milele) lakini sisi sote ni watoto wa Klabu ya YANGA, sisi ndiyo tunaoifanya YANGA kung’ara zaidi na sote lazima tujitolee. Kuna uamuzi niliufanya miaka 11 iliyopita, kuwa sisi ndio tutakao iokoa Klabu yetu na wakati huu ukiwa ni kweli tutaifanya Klabu yetu iwe bora kwa pamoja, niliutuma moyo wangu mbele kwa hiyo YANGA ilifahamu kuwa bado kuna mtu anauamini umoja wetu, anajali kwa kujitolea kwa YANGA na angethubutu kwa upendo wa YANGA yetu kuizuia isishindwe kwa kupigania ushindi wake.

Kama Mungu alivyotuonyesha kwa kubadili jiwe kuwa mkate, hivyo msaada wangu kwa uwezo wa neema zake, naamini ulifanya mabadiliko chanya na Klabu iko imara na huru. Lakini umefika wakati wangu wa kuachia wengine na wengine wasifikirie nilikuwa Kiongozi aliyetaka cheo chochote au umashuhuri, ila upendo uliomgusa kuitumikia Yanga yetu. Pamoja tulifanikiwa mengi sana, na kuandika historia ndani ya YANGA na nilipokea baraka zenu mimi binafsi na familia yangu kupitia furaha japo ndogo, iliyoweza kuwaletea , ambayo ninawashukuru sana.

Nilisema tokea mwaka 2014, kuwa sitagombea katika Uchaguzi wa Uongozi kwenye nafasi yoyote ndani ya Klabu na nikaonyesha mfano kuwa Klabu yetu siyo ya mtu mmoja ila ni yetu sote, na uongozi ni lazima utoke kwenye uchaguzi kwenye kizazi kimoja kwenda kingine.

 Lakini mwaka jana tulikuwa katika mashindano ya mabara (Continental Championships) na kucha pengo isingekuwa sahihi, hivyo kinyume na msimamo wangu niligombea uenyekiti wa YANGA na kupata ushindi bila kupingwa, lakini kama nikiendelea nitakuwa ninaonyesha mfano upi kwa watoto wetu – ambao wanaipenda YANGA kwasababu yetu? Kwani YANGA siyo Klabu yao kama ilivyo yenu na mimi?

Muda wangu wa kutangaza kuwa ninakaa pembeni kutoka kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga ni sasa – tayari tumekuwa mabingwa wa mashindano tena, tuna kikosi kizuri cha wachezaji na Makocha, tumeungana kwa umoja haijawhi kutokea , tumerudisha heshima ya kuwa washindani wa kweli katika Vilabu vya Afrika, na kuwa imara zaidi kiuchumi na mkataba wa ufadhili wa Sports Pesa n.k Nafahamu kuwa bado kuna mengi yanayohitajika, lakini barabara ya mambo yanayotakiwa kutimizwa haiwezi kuisha na siwezi kuwa mroho kwa kuamini kuwa mimi pekee nitakayeweza kutufikisha mwisho wa safari.

 Muda wangu kama Mwenyekiti wa Klabu yetu ulikuwa umeongezwa tu na haikumaanisha katika demokrasia yetu uwe ni ule usiokuwa na kikomo.

Kupitia taarifa hii, kutoka 20 May 2017 – Mimi Yusufali Mehbub Manji nimeachia ngazi kama Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club na Makamu Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club atakuwa Mwenyekiti wa Club mpaka hapo uchaguzi utakapofanyika kujaza nafasi ya Mwenyekiti.

Nawashukuru wale wote ambao wamekuwa na imani kwangu na natumaini kwamba matarajio ambao sikuweza kuyakamilisha, wafuasi wangu wataweza kuyakamilisha na mengine mengi zaidi.

No comments