PEMBEZONI

Post Top Ad

.

.

Tuesday, June 13, 2017

12:41 PM

Wanahabari wapigwa msasa kuhusu Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala boraMwandishi wa habari wa gazeti la Zanzibar Leo ( Zanzibar), Mwinyimvua Abdi Nzukwi akichangia mada katika mafunzo ya siku tano ya Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala bora yanayofanyika katika hotel ya Flomi mjini Morogoro na kuratibiwa Umoja wa KLabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)

Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu, Demokrasia na Utawala bora, Wakili Juma Thomas akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo ambao ni wanahabari kutoka mkoa mbalimbali nchini, mafunzo hayo yanaratibiwa na Umoja wa Klabu za Waandishi Tanzania (UTPC)

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Haki za binadamu, Demokrasia na Utawala bora yanayofanyika katika hotel ya Flomi Mjini Morogoro, kutoka kushoto ni Tunu Herman (Majira - Mwanza) , Samweli Mwanga (Mtanzania - Simiyu) na Mussa Mwangoka (Pembezoni blog - Rukwa).
Wanahabari wengine, wakifuatilia mafunzo kutoka kushoto ni Asha Athumani (Mbeya) na Rhoda Ezekiel wa gazeti la Uhuru kutoka mkoa wa Kigoma.


Friday, June 9, 2017

3:16 PM

Mwanafunzi wa darasa la sita abakwa hadi kufa

'
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Kapanga iliyopo kata ya Katuma tarafa ya Mwese Wilaya ya Tanganyika, Veronica Lucas (13) amekutwa akiwa amekufa baada ya kubakwa na watu wasiojulikana na kisha mwili wake kutupiwa kwenye shimo la Kolongo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benedict Mapujila alisema tukio hilo la mauaji ya kikatili lilitokea juzi nyakati za saa 11 jioni kijijini hapo.
2:56 PM

Jela miaka 23 kwa kuvunja na kuiba


Mahakama ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imemuhukumu kwenda jela miaka 23 Mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26) baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mtuhumiwa kukiri kosa mahakamani.

Wednesday, June 7, 2017

3:07 PM

Risasi zarindima Machimboni Katavi.Na Walter Mguluchuma, Katavi

Vurugu kubwa zimetokea katika machimbo ya madini ya dhahabu ya Isumamilomo yaliyopo tarafa ya Nsimbo Wilayani Mpanda hali iliyosababisha walinzi wa mgodi wa machimbo hayo kufyatua risasi kadhaa hewani ili kuwatawanya wachimbaji wenye hasira kali.

Taarifa kutoka katika Machimbo hayo zinadai kuwa vurugu hizo baina ya wachimbaj wadogo wa madini ya dhahabu na walinzi wa mgodi wa machimbo zimesababisha kibanda cha ofisi cha kupimia dhahabu na kile wachokaa walinzi kuchomwa moto.
2:22 PM

Walimu Manispaa ya S'wanga wachachamaa wakidai haki yao.


Baadhi ya walimu wa shule za msingi katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, wameutaka uongozi wa halmashauri ya Manispaa hiyo kuwalipa fedha zao uhamisho haraka iwezekanavyo kama serikali kuu ilivyoagiza.

Walimu hao walisema hayo jana kwa nyakati tofauti mara baada katika ofisi za waandishi wa habari mjini hapa, ambapo walidai tangu wamepewa barua za uhamisho feb 28 mwaka huu hawajalipwa stahiki zao hadi sasa.
1:43 PM

Mwandishi RTD afariki dunia dunia na kuzikwa Katavi


Na Walter Mguluchuma, Katavi.

Mwandishi wa  zamani wa Radio  Tanzania (RTD) kabla ya kuwa shirika la Utangazaji (TBC) hivi sasa Lucas Matipa (77) amefariki  Dunia na kuzikwa huko wilayani Mpanda Mkoani Katavi.

 Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Padri Somoni Matipa alisema Lucas  alifariki  hapo  jana  jioni nyakati za saa 12:30 nyumbani kwao maeneo ya mtaa wa  Majengo Manispaa ya Mpanda.

Tuesday, June 6, 2017

4:42 PM

Mguu wa Twiga wawapeleka jela miaka 60


Mwandishi wetu, Katavi.

Mahakama ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imewahukumu kifungo cha jumla miaka 60 jela washtakiwa watatu waliokutwa na hatia ya kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo imeitolewa jana na hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya kuridhishwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande zote mbili za mashitaka.