Breaking News

Majambazi yaua, yapora fedha na dhahabu mkoani Katavi


Na Walter Mguluchuma, Katavi. 
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia machimbo ya madini ya dhahabu ya ifumile kijiji cha Isumamilomo tarafa ya Nsimbo Wilaya ya  Mpanda na kuua mchimbaji mmoja kwa kumpiga risasi na kujeruhi wengine watatu na  kupora dhahabu gramu 600 yenye thamani ya Sh milioni 1.5

Kamanda Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda aliwaambia wandishi wa habari kuwa tukio hilo la ujambazi lilitokea usiku wa kuamkia jana katika machimbo hayo ya madini. 
Alisema majambazi hao waliokuwa watatu   walifika katika machimbo ya dhahabu ya Ifumile kijijini hapo wakiwa wamefunika sura za kwa kofia maalumu (Maski) na kuanza kuwashambulia kwa risasi za moto wachimbaji na baadhi ya wanunuzi waliokuwepo eneo hilo.
Katika shambulio hilo waliweza kuwajeruhi vibaya kwa risasi wachimbaji wanne katika sehemu zao   mbalimbali za mili yao huku baadhi ya wachimbaji walikuwa kwenye eneo hilo  waliweza kusalimika baada ya kuwa wamekimbilia kwenye vichaka .
Kamanda  Nyanda, alimtaja aliyekufa kwa kupigwa risasi kuwa ni Sita   Kalyalya (34 ), Mkazi wa Bariadi  mkoani Shiyanga   ambaye alipingwa  risasi ya tumboni na mkononi aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda wakati akiwa anapatiwa matibabu .
Wengine  waliojeruhiwa ni Joseph  panya (34)    ambaye amereruhiwa vibaya kwenye bega la kushoto na mguu wa kulia, Mrisho Rashid (21) aliyejeruhiwa mguu na mkono wa kushoto na Masunju Nguli.
Kamanda Nyanda, alisema  majambazi hao watatu hao  baada ya kuwajeruhi wachimbaji hao waliweza kupora fedha Sh milioni 1.2 gramu 650 Zach madini na mashine mbili za kutafutia madini na kutokomea nazo.
Mara baada ya tukio  hilo polisi walifika kwenye eneo hilo, waliweza kuokota risasi 24 za moto na  maganda saba  ya  risasi zilizotumika za bunduki ya kivita aina ya AK 47.
Alisema jeshi la polisi mkoa wa Katavi bado linaendelea kuwasaka majambazi waliohusika kwenye tukio hilo na wametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa  kuwapatia taarifa zitakazowawezesha kuwatia nguvuni watuhumiwa wa tukio hilo.
Kaimu Mganga Mkuu  wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda, Dk. Masanja Masanja alisema marehemu Sita Kalyalya, alifariki muda mfupi baada ya kuwa ametolewa kwenye chumba cha upasuaji ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya kuunganishiwa utumbo wake mkubwa ambao likuwa umekatika kutokana na kupigwa risasi tumboni.
Alisema majeruhi Joseph Panya  na  Mrisho Rashid hao ambao walikuwa wamelazwa katika wodi namba moja wamepewa rufaa na wamesafirishwa kwenda katika hospitali ya Rufaa ya muhimbili kwa  ajili ya matibabu zaidi  baada  ya hali zao kuwa  mbaya sana ambapo majeruhi Masunju Mgelu  yeye   amebaki  kwenye hospitali  hiyo, huku  hali yake  ikiwa inaendelea vizuri.

1 comment:

  1. The best titanium bar for the best craftsmanship in an
    In titan metal the titanium wood stove first how strong is titanium year alone, this award-winning table, designed in titanium exhaust collaboration with titanium curling iron Steve Wynn and his eponymous team at the Wynn Macau, earned the crown.

    ReplyDelete