Breaking News

Waislamu kufanya maandamano makubwa Sumbawanga.

Mwandishi wetu, Rukwa.


Waumini wa dini ya Kiislamu mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, wamepanga kufanya maandamano makubwa ya amani kushinikiza uongozi wa mkoa kubadili uamuzi wake wa kuzuia wasiendelee na ujenzi wa nyumba ya ibada katika eneo la bomani mjini hapa.
Shekhe Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Rashid Akilimali akizungumza jana mara baada ya kuendesha ibada nje ya jengo la msikiti   mbalo ujenzi wake umezuiwa uongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, kwa madai ya kutofuatwa kwa baadhi ya taratibu.

Pamoja na kufanya maandamano hayo, pia wamekubaliana kususia shughuli zote za kiserikali ambazo mkuu wa mkoa huo, Joachim Wangabo atashiriki wakidai yeye ndiye alishinikiza kuzuia msikiti huo usiendelee kujengwa kwa madai ya kutofuatwa kwa taratibu

Shekhe mkuu wa mkoa wa Rukwa, Rashid Akilimali alisema hayo jana mara baada ya kuendesha ibada katika msikiti huo ambao ujenzi wake bado haujakamilika, ambapo alidai kusikitishwa na zuio la kutoendelea kujengwa kwa msikiti huo wakati taratibu zote zinazotakiwa zimefuatwa.

Alisema wao hawana imani na mkuu wa mkoa wa Rukwa, Wangabo kwa kuwa yeye ndiye aliyeshinikiza kutolewa kwa zuio hilo la ujenzi wa msikiti wakati wakuu wengine wa mikoa waliopita wakujishughulisha na ujenzi wa msikiti huo.

Naye, Shekhe wa wilaya, Rajabu Stima alisema kuwa wao wametimiza vigezo vyote ikiwa pamoja na kuweka mabango ya kuonyesha eneo hilo unajengwa msikiti lakini jambo la kusikitisha wakati nyumba hiyo ya ibada ujenzi wake ukielekea kukamilika limekuja zuio la kutoendelea na ujenzi.

Alisema licha ya kumfuata mkuu wa mkoa kwa mazungumzo lakini kiongozi huyo wa serikali ameshikilia msimamo wake wa kutaka wasiendelee na ujenzi huo kwa madai wanapaswa kuheshimu zuio hilo lililotolewa na uongozi wa manispaa ya Sumbawanga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Njovu alikiri uongozi wa halmashauri hiyo umetoa zuio la kutoendelea na ujenzi huo lilitolewa zaidi ya juma moja lililopita baada ya baadhi ya wenyeviti wa mitaa kupeleka malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa.

Alisema katika malalamiko hayo walidai kwamba ujenzi wa msikiti katika eneo lile umekiuka sheria ya matumizi ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.

Njovu alisema jumuiya ya Istiqaama Sumbawanga ndio iliyoomba kibali cha kujenga msikiti katika eneo hilo ambapo hatua za awali za kubadilisha eneo hilo kutoka makazi  hadi kujenga nyumba za ibada walizifuata.

Alisema wakati wakisubiri kupata kibali hicho kutoka kwa kamishina wa ardhi, wamekuwa wakiendelea na ujenzi hali iliyowafanya wenyeviti hao kumweleza mkuu wa mkoa ambaye aliagiza halmashauri ya manispaa kutoa zuio hadi watakapopata kibali hicho lkutoka kwa kamishina wa ardhi.

Ujenzi wa msikiti huo umeanza tangu mwaka 2010, ambapo wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ndio imekuwa ikisuasua kutoa kibali hicho hadi sasa.

No comments