Waandishi wajeruhiwa Katika ajali ya gari
Waandishi watatu wamejeruhiwa katika baada ya gari aina Land Cruiser kuacha njia na kudumbukia kwenye Kolongo lililokuwa kando ya barabara ya Ilemba kuelekea Kalambanzite wakati wakitoka ziarani na mkuu wa mkoa wa Rukwa.
Waandishi waliojeruhiwa ni Willroad Sumia wa kituo cha Channel 10 ambaye anadai kupata maumivu makali sehemu za kichwa, ambapo amelazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU) Katika hospitali ya mkoa wa Rukwa.
Wengine ni Juddy Ngonyani (Azam TV) na Peti Siyame (Dailynews) ambao waliruhusiwa mara baada ya kufika hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa mmoja wa majeruhi hao, Juddy Ngonyani, ajali hiyo imetokea nyakati za mchana katika kijiji cha Ilembo wilayani Sumbawanga, Rukwa ambapo wanahabari hao walikuwa kwenye msafara wa mkuu wa mkoa wa Rukwa ambaye alifanya ziara ya kikazi eneo la Ilemba bonde la ziwa Rukwa.
Inadaiwa wakiwa njiani kuelekea mjini Sumbawanga dereva wa gari walilokuwa wamepanda wanahabari hao wakiwa na watendaji wengine wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya alilikwepa kugongana na Lori la mizigo.
Pia gari hilo lilinusurika kugonga mti akiwa katika mwendo wa kasi ndipo aliingia kwenye Kolongo na gari hiyo kupinduka.
Licha ya wanahabari hao, baadhi watendaji wa serikali walipata majeraha ni kaimu Mganga mkuu wa mkoa, Emmanuel Mtika na Katibu uenezi wa CCM mkoa wa Rukwa, Clement Bakuli ambao nao wamepumzishwa hospitalini hapo wakipatiwa matibabu.
No comments