Breaking News

Sugu na Mwenzake waenda jela miezi mitano.

 https://4.bp.blogspot.com/-hThJbsLacBg/WKc0R_cBL7I/AAAAAAAAFJ0/HOqXVWx0YLw_7abTCux8Rem_Jaeio4RkwCLcB/s1600/IMGL5946.JPG
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wahukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite alisema leo mahakani hapo kuwa washitakiwa wamekutwa na hatia kutokana na makosa waliyonayo.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika 30, 2017 katika viwanja vya shule ya msingi Mwenge jijini Mbeya.

2 comments: