Kijana aenda jela miaka 23 kwa hatia ya wizi
Mwandishi wetu
Katavi.
Mahakama ya Wilaya Mlele mkoani Katavi imemuhukumu Omary Ally (20) kifungo cha miaka 23 jela baada ya kupatikana na kosa la kuvunja na kuiba nyumbani kwa Ofisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mlele, Teothimu Swai baada ya mshitakiwa kukili makosa mawili aliyosomewa mahakamani hapo ya kuvunja na kuiba.
Awali katika kesi hiyo, mw endesha mashitaka mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongela al idai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo machi 29 mwaka huu nyakati za saa tisa usiku nyumbani kwa ofisa wa serikali.
Inadaiwa kwamba, siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alivunja nyumba ya afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Afred Sungura,kisha aliiba Laptop moja.
Mshitakiwa huyo baada ya kusomewa mashitaka hayo mawili alikiri Mahakamani hapo kutenda makosa hayo kwa makusudi, kwa madai alipitiwa na shetani tu ndio maana akalazimika kufanya wizi huo.
Hakimu Mkazi Swai alimhoji mshitakiwa huyo iwapo ana sababu ya yoyote ya kujitetea ili kuishawishi mahakama impunguzie adhabu.
Katika utetezi wake mshitakiwa, aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa bado ana umri mdogo wa miaka (20) maombi hayo ambayo yalipingwa vikali na mwendesha mashitaka, Hong ela na kuiamba mahakama itoe adha bu kali kwa mshitakiwa ili kukomesha watu wengine wenye tabia kama h iyo.
Hakimu Swai baada ya kusikia tetezi huo alimhukumu mshitakiwa huyo kwenda kutumikia kifungo cha miaka 23 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine.
No comments