RUKWA PRESS CLUB WALAANI POLISI KUZUIA MAANDAMANO YAO.
Na Mwandishi wetu.
WAANDISHI wa habari mkoa wa Rukwa, wamelaani hatua ya jeshi la polisi kuzuia maandamano yao yaliyopangwa kufanyika jana sambamba na waandishi habari wa mkoa mbalimbali nchini.
Maandamano hayo yalilenga kulaani mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daudi Mwangosi aliyeuawa na polisi katika vurugu zilizowahusisha polisi na wafuasi wa Chadema.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa mkoa wa Rukwa, Mussa Mwangoka,alisema kuwa hatua ya polisi mkoa huo kuwazuia waandishi kuandamana uendelezaji wa kutumia sheria kandamizi na zilizopitwa na wakati pasipo kutumia busara.
"tulitakiwa kutoa taarifa saa 48 kabla, lakini wakati mwingine walipaswa kutumia hekima na busara kuruhusu maandamano yetu, ambayo barua tuliowaandikia ilieleza bayana kwamba yalikuwa ya amani na yangehusisha wanahabari pekee" alisema.
Mwangoka alisema kuwa baada ya polisi kutotumia busara na kuwazuia kufanya hivyo hawakuona sababu ya kulazimisha kuandamana kwani hali hiyo ingeweza kuhatarisha amani kitu ambacho kingeichafua tasnia ya habari.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo waandishi hao wameazimia kwa kauli moja kutoandika habari zozote zinazohusu polisi hadi hapo watakapoona tume huru ya kuchunguza mauaji ya mwandishi huyo itakapoundwa, pia waone hatua zinachukuliwa kwa wale wote waliohusika katika mauaji hayo ndipo watakapoanza kushirikiana na polisi na si vinginevyo.
Alisema kuwa RKPC inaungana na waandishi na wafanyakazi katika tasnia ya habari nchini pamoja na Umoja wa Klabu za Waandishi nchini (UTPC) kulaani kwa nguvu zote matumizi ya mabavu ya polisi ambayo yamesababisha kifo cha mwandishi wa habari akiwa kazini na pia akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Kwani huo ni mwendelezo wa matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayofanywa na baadhi askari katika jeshi la polisi kwa raia wa nchi hii.
Mwisho.

No comments