Breaking News

MATUMIZI YA MASHINE ZA KISASA KUONGEZA MAKUSANYO YA KODI - TRA RUKWA.


Meneja wa TRA mkoa wa Rukwa, Philipo Kimune akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kuhusu wiki ya mlipakodi iliyoanza leo, kwa taar.ifa
IMEELEZWA kuwa upo uwezekano mkubwa kwa mamlaka ya mapato nchini (TRA) kuongeza makusanyo ya kodi ya mapato kutoka kwa wafanyabiashara wa kati iwapo watahamasika na matumizi ya mashine za kutolea stakabadhi ya manunuzi ya bidhaa.

Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Rukwa, Philipo Kimune alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu uzinduzi wa wiki ya mlipakodi iliyoanza leo na kufikia kilele chake Novemba 8 Mwaka huu.

Kimune alidai kuwa manufaa yatokanayo matumizi ya mashine hizo ni pamoja na kuwepo kwa uwezekano wa kuongeza makusanyo kutoka katika kundi la wafanyabiashara wa kati ambapo mara nyingi wamekuwa wakikwepa kulipa kodi.

Alisema kuwa pia matumizi hayo yatapunguza kama si kuondoa kabisa usumbufu uliopo sasa wa wafanyabiashara kufuatwa fuatwa na maofisa wa TRA na badala yake malipo ya kodi ya mapato yatafanyika kwa njia ya mtandao.

Mkutano ukiendelea kati ya waandishi wa habari na watumishi wa TRA kuhusu siku ya mlipakodi sherehe zilizoanza leo na kuhitimishwa Novemba 8 Mwaka huu.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia kwa makini maelezo ya ufunguzi wa wiki ya mlipakodi leo wakati yakitolewa na meneja wa TRA mkoa wa Rukwa.

No comments