MPASUKO WANUKIA CHADEMA S'WANGA
M/kiti CDM Mkoa, Zeno Nkoswe |
Mazingira hayo yanatajwa kwamba yanaweza
kukisambaratisha Chama hicho, ambacho kimeanza kukubalika na kujizolea
viti kadhaa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita, hali ambayo
imeonyesha kuwa ni tishio kwa CCM katika uchuguzi mkuu ujao wa Rais,
Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mmoja wa wanachama wa Chadema, Datus Sikazwe alisema kuwa baadhi ya viongozi (majina yanahifadhi) wenye uwezo wa kufanya maamuzi ndani ya Chadema wamekuwa wakimkumbatia mgombea mmoja wenye uwezo wa kiuchumi na kumuandalia mazingira ya kumteua kuwa mgombea ubunge kupitia Chadema katika jimbo hilo, hali ambayo inaweza kusababisha mgogoro mkubwa na hatimaye kukisambaratisha chama hicho katika siku zijazo.
"Unajua kila mtia nia iwe Ubunge au Udiwani ana makundi yake, sasa haingii akilini kila katika mikutano ya Chadema, viongozi wanaambatana na mgombea mmoja (mwenye fedha)kisha wanampa fursa ya kupanda jukwaani na kumdani kuwa ndio mgombea ubunge wakati yeye ni mtia nia tu ya ubunge, kama walivyo watia nia wengine ambao hawataki kuambatana nao katika mikutano hiyo wala kuelezea kwamba kuna idadi kadhaa ya watia nia......maana yake ni kwamba huyu anandaliwa mazingira ya kuteuliwa kitu ambacho ni kibaya na kinaweza kutugawa na wenzetu wakapata mwanya wa kutushinda katika uchaguzi mkuu ujao" alisema.
Aidha Blog ya Pembezonikabisa imebaini kuwa kundi la mmoja wa watia nia ya ubunge, Emmanuel Msengezi ambaye ni kijana mzawa na msomi ndio limekuwa likilalamika kwamba uongozi wa Chadema unandaa mazingira ya kuteua jina la Sadriki Malila ambaye ni mfanyabiashara maarufu kwa jina la IKUWO amekuwa akishirikishwa katika kila kitu na uongozi huo hali ambayo inatafsiriwa kuwa ni kumuandaa kuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo.
Taarifa
zinaeleza kuwa wafuasi hao wa Msengezi wanadaiwa kupeleka malalamiko
hayo kwa wazee wa Chadema wa Sumbawanga mjini wakiwataka kukaa na
uongozi huo ili kuwasihi waache kutengeneza mazingira ya kuwakatisha
tamaa watia nia wengine hali ambayo inaweza kusababisha kujitoa ili mtia
nia huyo abaki peke yake na kuteuliwa kugombea ubunge.
Hata
hivyo, Msengezi alipoulizwa kwa njia ya simu hakuwa tayari kuzungumzia
lolote kuhusu sakata hilo kwa madai kwamba kwa sasa yupo safarini
kikazi.
Mmoja wa Wazee hao,Norbert Yamsebo,
ambaye aligombea ubunge mwaka 2010 na kuangushwa na Aeshi Hilaly,
alikiri kukutana na mwenyekiti wa Chadema lakini hakuwa bayana kueleza
kile walichokijadili lakini alidai kulikuwa na malalamiko mmoja wa watia
nia ya ubunge.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Rukwa, Zeno Nkoswe licha
kukiri kufanya mazingumzo na wazee ambao ulikuwa sehemu ya ujumbe kutoka
kwa mmoja wa watia nia ya ubunge lakini alidai kwamba Chama hicho
hakipo tayari kukumbatia watu ambao wanakiuka utaratibu tuliojiwekea.
"Kuna
utaratibu tumeweka kwa watia nia ya ubunge na udiwani kwamba watakuwa
wakishiriki kwenye shughuli zote za ujenzi wa Chama sasa kuna baadhi
hawataki badala yake wanafanya kampeni nyakati za usiku......tena
kampeni za ukabila sasa sisi katika chama kampeni za hivyo hazina
nafasi" alisema Mwenyekiti huyo
Aliongeza
kuwa Chadema ipo imara kwa sasa na wanajipanga kuweka watu ambao
watakuwa sahihi kugombea ubunge ili waweze kufikia malengo yao ya
kuchukua majimbo yote matano ya mkoa wa Rukwa.
Hata
hivyo mmoja wa viongozi wa juu ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake
alisema kuwa ni wazi Chadema tayari imemteua Ikuwo kugombea ubunge
katika jimbo hilo kwa kuwa amekuwa na mchango mkubwa wa kifedha katika
ujenzi wa Chama kuliko wagombea wengine ila kinachofanyika sasa ni
utaratibu tu.
No comments