Breaking News

Hakimu agoma kujitoa kesi ya Sugu na Masonga

Mwandishi wetu, Mbeya 

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite amekataa kujitoa kusikiliza kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na mwenzake.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli wanayodaiwa kuitoa Desemba 30, mwaka jana.

Mapema jana Sugu na Masonga waliwasilisha ombi mahakamani wakimkataa hakimu huyo wakitaka ajitoe kusikiliza kesi kwa maelezo kuwa hawana imani naye.

Hakimu Mteite amesema sababu zilizotolewa na akina Sugu hazipo kisheria na hazimfanyi kujitoa.

Baada ya hakimu kukataa kujitoa, mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo wanaowawakilisha washtakiwa walitangaza kujitoa katika shauri hilo.

Sugu na Masonga wameiomba Mahakama kuwapatia wiki mbili za kutafuta mawakili wengine.

Hakimu Mteite ameahirisha kesi hadi Februari 2 mwaka huu, na ameamuru washtakiwa kurejeshwa rumande.

No comments