WANAHARAKATI , WADAU WALAANI BAA KUJENGWA ENEO LA SHULE.
Moja ya baa inayouza vileo ambayo imejengwa katika eneo la shule ya Sekondari Mazwi iliyopo mjini Sumbawanga. Picha na Peti Siyame.
Mussa Mwangoka, Sumbawanga.
WANAHARAKA na wadau wa elimu wamelaani uamuzi uliofanywa uongozi wa shule ya Sekondari ya Mazwi iliyopo mjini Sumbawanga kwa kuruhusu ujenzi wa baa na maduka ya kuuzia vileo kwenye eneo la shule.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wadau hao, walisema kuwa hatua ya uongozi wa shule hiyo kuruhusu ujenzi wa baa moja kubwa na maduka ya vileo saba katika eneo la shule kusababisha kuwapo kwa mmomonyoko wa maadili miongoni mwa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo.
Mmoja wa wadau hao wa elimu ambaye ni Katibu wa Chama cha walimu (CWT) mkoa wa Rukwa, Tweedsmuir Zambi, alisema kuwa pamoja na kwamba shule hiyo ni ya kutwa lakini kutokana kufanyika kwa biashara za kuuza pombe katika uzio wa unaozunguka shule hiyo, kutasababisha wanafunzi wa kike kushawishika kirahisi hivyo kupata ujauzito.
Alisema kuwa pia wanafunzi hao wapo katika hatari ya kujiingiza kwenye ulevi na watoro hali ambayo inaweza kusababisha washindwe kufuatilia masomo yao pindi wawapo darasani, kupata matokeo mabaya katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari.
"Katika hali hiyo ni vigumu sana kwa walimu kuwadhibiti wanafunzi hao kinidhamu hivyo moja kwa moja wanafunzi hao watakosa malezi bora, wengine watashindwa hata kumaliza elimu ya sekondari kutokana na mazingira hayo kutokuwa rafiki kwa wanafunzi hao" alisema Zambi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya katuma ya mjini hapa, Japhet Nzalamte, akitoa maoni yake, alisema kuwa uongozi wa shule hiyo kama ulilenga kujipatia kipato kupitia maduka ya biashara yanayozunguka uzio wa shule hiyo, walipaswa kuruhusu ifanyike biashara ambayo hawezi kuathiri ukuaji na ustawi wa maendeleo ya mtoto kielimu.
Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Reginald Kauzeni, pamoja na kukiri udhaifu huo, aliongeza kuwa wao inawawia vigumu kudhibiti nidhamu ya wanafunzi hao kutokana na kufanyika kwa biashara hizo ambazo si rafiki na mazingira ya shule.
"mimi nimeamia mwanzo mwa mwaka huu hapa shuleni na nimekuta biashara hii ikiendelea kufanyika..... tumechukua hatua za kuutaarifu uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga ili waweze kudhibiti ufanyikaji wa biashara hii kwa hiyo tunasubiri kuona hatua zikichukuliwa lakini hali hii hatufurahishi hata kidogo" alisema Mwl. Kauzeni.
Mkuu huyo wa shule alifafanua kuwa wamiliki wengine wa baa na maduka hayo ya vileo ni watumishi wa Manispaa akiwamo mkuu wa idara ambaye ni mhandisi wa ujenzi Baraka Mkuya anayedaiwa kuandaa michoro ya uzio huo wa shule.
Akihojiwa na waandishi wa habari ofisi kwake, Mhandisi Mkuya, akiri kuwa ni mmoja wa wamiliki wa baa maarufu iitwayo The Place Pub iliyopo katika eneo hilo la shule, alidai kuwa hakuandaa mchoro ila uliandaliwa na uongozi wa shule, wao (uongozi wa Manispaa) wakaidhinisha.
Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Sabas Katepa, alisema kuwa tayari wameaandikia barua watu wote wanaofanya biashara za kuuza vileo na biashara nyingine zinazoweza kuwaathiri kielimu wanafunzi kuondoka katika eneo hilo.
Ujenzi wa maduka ya biashara katika eneo hilo umeanza taratibu mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo hivi karibuni maduka na baa zimeanza kujengwa kwa kasi kubwa huku zikiwa hazina vyoo hivyo kuzagaa kwa vinyesi na harufu ya kuchukiza ya mikojo hali ambayo inaweza kusababisha kutokea kwa ugonjwa wa mlipuko.
Mwisho.

No comments