Breaking News

MKAZI WA MPANDA AENDA JELA KWA KUTAKA KUMBAKA MAMA YAKE MZAZI

Peti Siyame, Sumbawanga

MAHAKAMANI ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa  Rukwa  imemuhukumu  Ernest Fredrick  (38),  mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa Migazini  mjini  humo ,kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kutaka  kumbaka mama yake mzazi.

Mwendesha Mashtaka  Mkaguzi  wa Polisi,  Timoth   Nyika,  alidai   mahakamani hapo  kuwa  mshitakiwa  alitenda kosa hili  Septemba 29, mwaka  jana  nyumbani kwa mama yake mzazi .

Ilidaiwa  mahamani  hapo  mbele  ya Hakimu  Mkazi Mfawidhi  wa Mahakama  hiyo  Richard Kasele,  ya  kuwa siku hiyo mshitakiwa aliingia ndani ya nyumba ya mama yake na kisha kumshika kwa nguvu kwa lengo la kufanya naye mapenzi.

Kesi  hiyo  iliyovuta hisia za watu  wengi  mjini  hapa  ilidaiwa  mahakamani hapo kuwa mama huyo licha ya kukataa  kufanya  mapenzi mwanae huyo  bado aliendelea kumshika kwa nguvu na kumvua nguo mama yake  huyo  mzazi.

“Baada ya kuona hali hiyo mama huyo alipiga mayowe ya kuomba msaada Kwa majirani ambao walifika katika nyumba ya mama huyo na kumkuta mwanae akiwa amemlalia huku akiendelea kuomba msaada……..

‘Majirani hao waliweza kumwokoa mama huyo na kisha  aliwapa maelezo ya kuwa mwanae alikuwa anamshika kwa nguvu na kumlazimisha wafanye nae mapenzi baada ya maelezo majirani waliamua kumkamata   mthumiwa na kumpeleka katika Kituo   cha Kati   ch Polisi  mjini  humo ‘  alisema  Nyika .

Hakimu Kasele alisema  kuwa  ameridhika  na  ushahidi   uliotolewa  na  upande  wa mashtaka kuwa  pasipo  kutia  shaka  yeyte  kuwa  mshtakiwa  alitenda  unyama  huo  ..

Baaada ya Hakimu  Kasele  kusikiliza pande hizo mbili za mashitaka ambapo u upande  wa  mashtaka  ulileta  mashahidi   wawili  miongoni  mwao  akiwa  mama  yake  mzazi  mabapo  upande  wa   utetezi  haukuwa  na  shahidi  yeyote  , alimtia  mshitakiwa hatiani.

Mshitakiwa alipoombwa  na  mahakama  hiyo  ajitetee  aliomba apunguzie adhabu kwani yeye bado nikijana hata hivyo ombi hilo lilipingwa vikali na mwendesha mashitaka kwa kile alichodai kama mshitakiwa  aliweza  kufanya  nyama  huo  kwa mama  yake  mzazi  kwa watu  wengine  itakuwa  ni   balaa .

Hakimu Kasele  alisema Mahakama imemtia hatiani  mtuhumiwa  hivyo anahukumiwa kwa kosa la kuvunja sheria No. 158 (1.B) 3 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002 ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 jela, haa  hivyo   haikuwezakufahamika  mara  moja  kama  takata  rufaa  au  laa.

Mwisho.

No comments