POLISI WATIMULIWA KAZI KWA KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
![]() |
| Mkuu wa Jeshi laPolisi nchini, IGP,Said Mwema. |
JESHI la polisi mkoa wa Rukwa, limewafukuza kazi askari wake wawili na kuamuru wafikishwe mahakamani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh 144 milioni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage, alisema jana kuwa polisi ilitoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa katika mahakama ya kijeshi kufuatia makosa mawili yaliyokuwa yakiwakabili askari hao ambao ni G. 2874 PC Fredrick na G. 9116 PC Venance.
Kamanda Mantage alisema kuwa askari hao walitenda kosa hilo Novemba 11 mwaka huu, saa tano usiku wakati wakiwa zamu katika chumba cha mashtaka katika kituo kikuu cha polisi wilaya ya Mpanda ambapo walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kwenye gari liitwalo Adventure Connection linalofanya safari kati ya Mpanda na Kigoma kuna abiria amebeba mzigo wa meno ya Tembo.
Alisema kuwa kufuatia taarifa hiyo, askari hao bila kumjulisha kiongozi wao yoyote walielekea eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa huyo pamoja na meno ya tembo lakini katika mazingira ya kutatanisha wakati wakiwa njiani kumpeleka kituoni walimwachia mtuhumiwa huyo na kuendelea na kazi bila kutoa taarifa kwa kiongozi wao yoyote.
Aliongeza kuwa siku iliyofuata ofisa wanyamapori wilaya ya Mpanda aliyefahamika kwa jina moja la Mushi alipata taarifa kuwa kuwa ndani ya basi hilo ambalo tayari lilikuwa limeanza safari kuelekea Kigoma kuna kuna abiria amebeba meno ya tembo ambapo aliwatuma askari kufukuzia basi hilo na kufanikiwa kulikuta maeneo ya Mishamo umbali wa kilometa 140.
Inadawa kuwa polisi hao walifanya upekezi katika gari hilo na kukuta vipande 13 vya meno ya tembo vikiwa kwenye begi moja lililokuwa kwenye buti la gari hilo na walipohojiwa abiria ili kujua mmiliki wa begi hilo hakuna aliyejitokeza hivyo iliwalazimu askari hao kumkamata mhudumu wa gari hilo aliyekuwa na jukumu la kupakia mizigo kwenye buti la gari hilo.
Hata hivyo uchunguzi wa shauri hilo ulipofanyika iligundulika kuwa siku moja kabla ya siku hiyo tayari askari hao wawili walikuwa wamepata taarifa na kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa na nyara hizo kisha kumuachia katika mazingira tatanishi ambapo askari hao walikamatwa na kuhojiwa walikiri kumkamata mtuhumiwa huyo.
Inasemekana kuwa wakiwa katika harakati za kumfikisha kituo cha polisi mtuhumiwa huyo aliyekuwa na meno manne ya tembo aliwatoroka na kukimbilia kusikojulikana.
Aidha walipohojiwa kwanini hawakutoa taarifa kwa viongozi wao walishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha lakini walipopekuliwa katika nyumba wanazoishi walikutwa na vipande vinne vya meno ya tembo ambavyo ukilinganisha na vile vilivyokutwa kwenye gari vilionekana kuwa sawa na kufanya idadi yake kuwa 17 ambavyo ilibainika kupatikana baada ya tembo sita kuuawa.
Mwisho.

No comments