WAFUNGWA GEREZA LA MAHABUSU SUMBAWANGA WAPATIWA MSAADA
WANANCHI wa mkoa wa Rukwa kuwa mstari wa mbele kama ilivyo kwa taasisi za kidini katika kuisaidia jamii ya watu wenye mahitaji mbalimbali ili kuondoa dhana kwamba watu wa aina hiyo wametengwa miongini mwa jamii.
Wito huo umetolewa leo na Kamishina Msaidizi wa Magereza mkoa wa Rukwa, George Kiria mara baada ya kupokea msaada wa vyakula na sabuni kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa.
Alisema kuwa ni taasisi za kidini pekee ndizo zimekuwa zikiwakumbuka watu wenye mahitaji hususani wafungwa kitu ambacho wananchi wengine wanapaswa kuiga mfano huo ili watu hao wasijione kwamba wametenga na jami kitu ambacho kinawafanya baadhi yao kukata tamaa ya maisha.
" ni kweli wamefanya wamekosa lakini jamii hainabudi kuwakumbuka kwa kutoa vitu mbalimbali kwani wafungwa nao wanamahitaji kama ilivyo kwa watoto wa mitaani, yatima wazee na wagonjwa" alisema Kamishina Kiria.
Awali akitoa msaada huo, kwa niaba ya mkuu wa Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya, Ofisa habari wa mkoa huo, Hamza Temba, alisema kuwa lengo la msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Sh 300,000 ni kwaajili kuadhimisha sherehe za Mapinduzi inayoadhimishwa kitaifa Januari 12 kila mwaka.
Alisema kuwa uongozi wa mkoa umeona kuna kila sababu ya kuona wafungwa nao wanasherekea sikukuu hiyo kwani nao ni sehemu ya jamii kama ilivyo kwa watu wenginepamoja na kwamba wanatumikia kifungo gerezani.

No comments