Breaking News

MANISPAA S'WANGA YATAKIWA KUTUNGA SHERIA ILI KUWABANA WANAOZIBA VICHOCHORO.

BAADHI ya wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa, wameutaka uongozi wa manispaa hiyo kutunga sheria ndogo zitakazowabana baadhi ya wamiliki  wa nyumba za kulala wageni ambao wamekukiuka agizo lilowataka wasizibe vvichochoro zilivyopo kwenye nyumba zao.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti na mwandishi wa blog hii mjini hapa, wananchi hao walisema kuwa baadhi ya watu wanaomiliki wa nyumba za kulala wageni wamekiuka agizo la kutoziba vichochoro hivyo uongozi wa manispaa hiyo haupaswi kulifumbia macho jambo suala hilo.

Mmoja wa wananchi hao Samweli Malingumu, alisema kuwa uzibaji wa vichochoro umekuwa ukisababisha kero kwa watumiaji wa vichochoro hivyo lakini pia  athari zake zinaweza kujitokeza pindi yanapotokea majanga ya moto ambapo ni vigumu kwa watu wa zimamoto kuweza kuifikia nyumba ambayo inawaka moto ili watoe msaada wa kuzima.

"kuna kipindi Manispaa iliendesha zoezi la kuvifungua vichochoro vyote ambavyo vilizibwa, zoezi ambalo lilifanikiwa sana lakini sasa hawa watu wanaojenga nyumba za kulala wageni wanaziba vichochoro na kugeuza ndio maeneo ya kuegesha magari ya wageni wao wanaofikia katika nyumba hizo" alisema Malingumu.

Alisema kuwa ikiwepo sheria itawafanya watu wanaoziba vichochoro kuacha kufanya hivyo kwa kuwa sheria itafuata mkondo wake tofauti na sasa ambapo hakuna sheria inayowabana hivyo kujifanyia mambo vile ambavyo wanaona inafaa.

Naye Peter Maridadi, mkazi wa eneo la jangwani mjini hapa, alisema kuwa licha ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuziba vichochoro lakini pia kufanya hivyo inachangia kuharibu muonekano mzuri wa mji huo ambao umejengeka kwa kufuata mitaa.

Mji wa Sumbawanga ni miongoni mwa baadhi ya mji michache nchini iliyojengeka katika mpangilio mzuri lakini uzibaji wa vichochoro unaoendelea hivi sasa unatishia mji huo kuwa katika mpangilio mzuri kama ilivyokuwa awali.

No comments