Breaking News

MZINDAKAYA AFUNGUKA, ASEMA WALA RUSHWA NA MAFISADI HAWANA NAFASI CCM.

Dk. Chrisant Mzindakaya.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kurejesha imani kwa wananchi iwapo viongozi na wananchama wake wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi hawataruhusiwa kugombea nafasi zozote ndani ya chama hicho katika uchaguzi ujao wa CCM unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu.

Mwanasiasa Mkongwe na machachari nchini, Dk. Chrisant Mzindakaya,alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo alidai kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wananuka rushwa na ufisadi huku wakiwa wamechokwa na wananchi lakini wang'ang'ania kutaka kuendelea kuwepo madarakani.

Mwanasiasa huyo alisema kuwa kwa mtizamo wake anaona kuwa uchuguzi mkuu wa chama hicho utumike kuisafisha CCM ili kiweze kurejesha imani kwa wananchi na hatimaye kupata ushindi katika chaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"kwa wale ambao wananuka rushwa na ufisadi wang'atuke wenyewe, na wakikataa chama kiwaandikie barua ya kuwazuia kugombea kabla ya chaguzi za CCM kuanza katika ngazi zote kuanzia matawi hadi taifa........ na kama CCM itawaonea aibu na kuwapitisha yeye atakuwa tayari kujitokeza hadharani na kuwataja watu hao ambao ni vinara wa rushwa na ufisadi kwa kuwa wanafahamika ndani ya chama na wananchi wanawajua" alisema Mzindakaya.

Alisema kuwa wananchi wanapowanung'unikia inatosha kabisa kuwaengua madarakani haihitaji ushaidi kwa kuwa tayari wamefirisika kimaadili na wanapaswa kung'atuka katika nafasi walizonazo.

Aliongeze kuwa aliongeza kuwa rushwa iliyopo hivi sasa imelelewa na CCM yenyewe kwa kuwa kila kinapotokea uchaguzi baadhi ya viongozi wanatumia  rushwa kupata uongozi lakini malalamiko hayo yanapofikishwa ngazi za juu zenye maamuzi inadaiwa kuwa wote wametoa rushwa ila kwa kuzidiana.

"hakuna rushwa ndogo wala kubwa na hakuna ufisadi mkubwa wala mdogo........ uchafu huo haupimwi kwa wingi wa pesa mbona enzi ya mwalimu Julius Nyerere alikuwa na utaratibu wa kuwang'oa watu wote wanaotuhumiwa kwa rushwa hivyo wanachama wa CCM wanapaswa kutumia uchaguzi mkuu wa chama hicho unaokuja kuwang'oa watu hao" alisema Mwanasiasa hao.

Aliwaponda baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya nne hawana ufanisi kwani akili zao wamezielekeza kwenye mbio za urais badala ya kumsaidia rais Kikwete katika shughuli za kiutendaji wamekuwa wakipanga mikakati nani atakuwa rais  mwaka 2015 kitendo hicho ni ukosefu wa uadilifu wa kiuongozi.

Katika hatua nyingine, mwanasiasa huyo ambaye pia mjumbe wa kudumu wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Rukwa, alikemea tabia ya baadhi ya wanasiasa kutumia fedha kutafuta cheo cha urais kwani cheo hicho hakipaswi kutafutwa kwa pesa ila ni matakwa ya raia na baraka za mungu.

Alisema kuwa wanasiasa hao wanaotafuta urais kwa fedha wamekuwa kero kubwa kwa chama na taifa na akiendelea kufumbiwa macho watalipeleka taifa kubaya hivyo kama hitaji lao ni urais watumie nguvu ya hoja na wala si kutumia rushwa.

Mwanasiasa huyo huyo aliwalaumu baadhi ya wamiliki wa nyumba za ibada kuwaruhusu baadhi ya wanasiasa kutumia nyumba hizo kuhubiri siasa badala ya neno la mungu kitu ambacho ni makosa makubwa.

Pia alisema kuwa wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Sumbawanga mjini wamekichafua chama na wananuka rushwa hivyo wanapaswa kung'atuka wenyewe kabla wanachama hawajawaondoa madarakani kwani walipitisha wagombea ambao hawafai na hawana sifa.

No comments