WAUMINI WADAI MGOGORO WA KANISA LA ANGLIKANA SUMBAWANGA MBICHI.
ASKOFU Mkuu wa Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa. |
Kauli hiyo imekuja zikiwa ni siku chache tangu gazeti moja linalotolewa kila siku ambalo liliandika habari zilizodai kuwa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu wa umefikia muafaka baada ya kundi lililokuwa likipinga uwepo wa Askofu Mathayo Kasagala kukubali mazungumzo yafanyike nje ya mahakama.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viunga vya kanisa hilo la watakatifu wote lililopo mjini hapa, Mjumbe wa kamati ya kusimamia kanisa hilo Flugence Lusunzu, alisema kamati na waumini wa kanisa hilo na wale wa 'Parish' ya Kabwe, Kantalamba na Muze wameshtushwa na taarifa hizo ambazo amedai zina lengo la kuupotosha umma.
Lusunzu alisema kuwa mgogoro huo bado haujapatiwa ufumbuzi kama inavyoelezwa hadi hapo nyumba ya maaskofu itakapokutana na kuzikutanisha pande zote mbili kisha kutoa maamuzi.
"Sisi hatuna tatizo kuhusu muafaka ndio maana tumeondoa kesi mahakamani kutoa fursa ya utatuzi wa mgogoro huu..... lakini kinachatakiwa kufanyika hapa si kukimbia kwenye vyombo vya habari na kudai.... 'mgogoro Anglikana Rukwa wapata dawa' huo ni upotoshaji wenye lengo la kuharibu makubaliano yaliyofikiwa na pande zote mbili" alisema.
Alisema kuwa kamati inaeleza wazi kwamba kinachoendelea sasa ni kusubiri kikoa cha nyumba ya maaskofu ili kuona kama utatuzi wa mgogoro utatekelezwa kwa kufuata vipengele vya mkataba wa makubaliano ambayo yamesainiwa na pande zote mbili.
Lusunzu aliongeza kuwa pia kamati inakanusha sababu zilizotolewa na gazeti hilo kuwa chanzo cha migogoro ya kanisa ni hususani kanisa lao hazina msingi wowote na zinatolewa bila kufanya utafiti wa kina kujua chanzo cha migogoro hiyo.
katika gazeti hilo alinukuliwa, Katibu mkuu wa Anglikana Dk, Dickson Chilongani akieleza kwamba pamoja uamuzi huo washitaki wa Dayosisi hiyo wametoa sharti la kuzuia kwa askofu Kasagala kuingia kanisa kuu kwa ibada yoyote hadi ufumbuzi wa suala hilo upatikane.
Katika kesi hiyo mahakamani ya Hakimu Mkazi Sumbawanga, waumini wa anglikana, Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera na wenzao 191 walifungua kesi namba 11/2011 wakipinga kuchaguliwa kwa askofu Kasagala kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo.
Moja ya sababu walizoeleza ni kuwa askofu huyo alishinda kwa kutoa rushwa hivyo wasingekubali kuongozwa na mtoa rushwa ndani ya utumishi wake, ambapo maaskofu wa kanisa hilo wanatarajia kukutana mjini Arusha Machi 9 hadi 10 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine kutakuwa na ajenda hiyo.
Hata hivyo pia Katibu huyo anadaiwa kueleza kuwa kinachowasumbua waumini wengi ni kuamini katika nafasi ya uaskofu kuna mshahara mkubwa na malupulupu na kwamba inapelekea kuwapo kwa fujo nyingi katika uchaguzi.
No comments