Breaking News

WALIMU KIZIMBANI KWA WIZI WA MAMILIONI MPANDA.

Na WAlter Mguluchuma, Katavi.

WALIMU watatu wa shule ya msingi Tukoma katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi juzi wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Mpanda wakiwa na mzabuni wa halmashauri hiyo wakikabiliwa na mashtaka 68 kwa tuhuma za wizi ya zaidi ya Sh milioni 21.

 Waliosomewa mashtaka hayo 68 mbele hakimu mkazi mfawidhi, Richard Kasele, ni Joel Mwakyusa  (37) mwalimu mkuu wa shule ya Tukoma, Renatus Ngairo (50) Joackim Katabi (39)  walimu wa shule hiyo ya Tukoma pamoja na mzabuni wa kampuni ya Royal Stationary Fredrick Mlenge (50.)

Mwendesha mshtaka mkaguzi wa polisi Finias Majura alidai mahakani hapo kuwa washtakiwa hawa kwa pamoja walitenda kosa hilo novemba 28 2009 na Agust 28 2011 kwa nyakati tofauti

Miongoni mwa mashtaki 68 waliosomewa  ni kula njama za kumuiba mwajiri wao wakiwa watumishi wa serikali na kumdanganya mwajiri wao na kujipatia jumla ya Sh 21,800,000.

Pia wanadaiwa kutengeneza hati bandia ya kujipatia pesa kupitia benki ya NMB tawi la Mpanda kwa kutumia jina la mwalimu mkuu wa shule ya Tukoma kwa kutumia hundi namba 002490788 yenye thamani ya Sh. 850,000.

Mwendesha mashtaka Majura alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao watatu ambao ni walimu ya shule hiyo ya msingi kwa nyakati tofauti wakishirikiana na mzabuni wa kampuni ya Royal Stationary walishirikiana kumuiba mwajiri ambae ni halmashari ya wilaya ya Mpanda kiasi hicho cha fedha ambazo zilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule

Washtakiwa hao wanne baada ya kusomewa mashtaka hayo, walikana mashtaka hayo yote 68 ambapo hakimu mkazi Kasele aliamuru washtakiwa hao waende rumande hadi mahakama itakaposikiliza ombi lao la kutaka kupatiwa dhamana.

No comments