MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI, ILEMBA WAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA.
Mbunge wa Jimbo la Kwela, Ignas Malocha akimtwisha ndoo ya maji, Rose Simtowe juzi baada ya kuzindua mradi safi katika kijiji cha Ilemba katika wiki ya maji. habari zaidi soma hapo chini. |
Mbunge wa Jimbo la Kwela, Ignas Malocha alisema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ilemba , muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa maji katika maadhimisho ya wiki ya maji yaliyofanyika katika kijiji cha Ilemba.
Alisema kuwa kero ya maji ambayo inajitokeza hivi sasa katika maeneo mengi ni kutokana na kukithiri kwa uharibifu wa mazingira, ikiwa ni ukataji miti, uchomaji wa misitu hovyo na baadhi ya watu kulima katika vyanzo vya maji na kusababisha vyanzo hivyo kukaukaharibifu wa mazingira ambapo athari zake ni wananchi kukosa maji kwaajili ya matumizi mbalimbali.
Mbunge huyo alisema kuwa sheria hiyo ikitumika ndi suluhisho la kuepukana ukame ambao unajitokeza sasa katika maeneo mengi ambao ni sehemu ya athari kubwa ya mabadiliko tabia nchi yanayojitokeza katika nchi magharibi.
Kwa upande wake, Kaimu Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya, Habibu Salum alisema kuwa mradi huo umegharimu zaidi ya Sh 27 milioni utasaidia kupunguza kero ya maji katika vijiji vipatavyo saba katika kata ya hiyo inayoelezwa kuwa na vijiji 27.
Mbunge wa Jimbo la Kwela, Ignas Malocha akifungua bomba ya maji safi katika kijiji cha Ilemba juzi ikiwa ni sehemu ya kuzindua mradi wa maji katika wiki ya maji wilayani Sumbawanga mkoni Rukwa |
No comments