Breaking News

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII (PSPF) YAPIGA JEKI MBIO ZA MWENGE RUKWA.

Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Wakili Ileth Mawala akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya jumla flana 130 na Truck Suits 18 zitakazotumika kwenye shughuli ya kukimbiza mwenge Mkoani Rukwa. Mwenge wa uhuru utakimbizwa kuanzia Septemba 15-18, mwaka huu mkoani Rukwa. 

Mkuu huyo wa Mkoa alishukuru kwa zawadi hizo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo wa PSPF kwa kuchangia kwenye shughuli za maendeleo Mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla. Picha kwa niaba ya blog ya mkoa wa Rukwa.

No comments