NURU TOGWA, KIJANA ALIYEKATWA MASIKO BAADA YA KUPITA KWENYE SHAMBA LA KANISA.
Na Mwandishi wetu
WASWAHILI usema hujafa hujaumbika.....wakimaanisha kwamba katika safari ya maisha lolote linaweza kutokea kwaama ya kwamba umezaliwa mzima wa viungo vyote lakini pasipo mategemeo unapata ulemavu.
Si kitu kigeni katika maisha ya siku hizi, lakini kuna mazingira hata ukipata ulemavu wa kudumu inaweza isikuumize sana ila ikitokea unapata ulemavu katika mazingira ya uonevu, unyanyasaji na ukatili uliopindukia inaumiza sana.
Nuru Tongwa miaka 30 ni mmoja wa wananchi wa kijiji cha Malonje, ambaye kwa sasa ni mlemavu, baada ya kukatwa masikio yote mawili kwa wakati mmoja kutokana na kile kilichodaiwa alipita ndani ya shamba la Mifugo la DAFCO- Malonje mkoani Rukwa.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa tangu
Serikali ya mkoa wa Rukwa lilipouza shamba hilo lenye hekta 15,000 kwa gharama ya Sh milioni 600 kwa mwekezaji Nabii
Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha Ministry, ukatili wa aina hiyo dhidi ya wananchi ni jambo la kawaida.
Kijana huyo kwa sasa ni mlemavu kwa kuwa hawezi kusikia vizuri tangu
alipokatwa masikio yake, kwani unapozungumza naye inakulazimu utumie
sauti ya juu sana ndio aweze kukusikia.
katika mahojiano na mwandishi wa makala hii, anasema kuwa "Muda mrefu kidogo umepita........ ni zaidi ya miaka mitano (5) tangu nilipokutana na
ukatili huo ambao sitokuja kuusahau maishani mwangu......nilikuwa nikitoka Ziwa
Rukwa, ilikuwa ni asubuhi na nilikuwa nimebeba kikapu cha samaki wabichi
nikielekea mjini Sumbawanga.
Kuuza samaki hao maarufu kwa jina la hailali ambako ndiko kuna soko la bidhaa hiyo, lakini
nikiwa njiani kuelekea huko ghafla walitokea watu watano wakanisimamisha na
kuniamuru nikae chini, na kunitaka kutoa maaelezo ya kwanini nimepita kwenye
njia zilizopo shambani humo ili hali tayari kuna zuio?”.
Kabla ya kueleza lolote nilianza
kupata kipigo kutoka kwa wale watu ambao walikuwa ni walinzi shamba la Malonje ambao walikuwa na silaha za jadi kisha
kunichukua hadi kwenye kambi yao ambako nako niliendelea kupigwa.
Mwisho
walinifunga kamba na miguu halafu walichukua panga na kunikata sikio la kwanza
kisha kumalizia sikio la pili, hakika nilijisikia maumivu makali sana ambayo hayajawahi kutokea!, ambapo
damu nyingi zilivuja na kupoteza fahamu ndipo nilifikishwa polisi kisha
hospitali ya mkoa kwa matibabu, pasi kujitambua" alisema.
Togwa aliongeza kuwa baada ya kutoka hospitali aliwekwa rumande kwa kosa la kuiba ngano gunia 40 na siku iliyofuatwa alifikishwa mahakama ya mwanzo mjini Sumbawanga.
Ambako
kesi hiyo ilitajwa mara moja tu lakini baada ya hapo iliharishwa kwa
zaidi ya mara tisa kisha hakimu akaniachia huru kwa kuwa na upande wa
walalamika kutoudhuria mahakamani.
Baada ya Kukatwa masiko.
Togwa alisema kuwa baada ya kukatwa masikio na kesi kutoendelea mahakamani, hakujua wapi atakwenda kudai haki yake hivyo alishawishika kuwafuata watu wa kitengo cha haki za binadamu mkoa wa Rukwa na kuwaeleza kile kilichomsibu, lakini nao walishindwa kumsaidia kwa namna yoyote ile.
Alisema kuwa mchumba wake aliyetarajia kumuoa jina linahifadhiwa kwa sasa, alimkataa na hadi sasa hajawahi kupata mchumba wala mwanamke wa kumuoa hivyo anahisi kuwa mnyonge na asiye na thamani tena ndani ya jamii.
Tongwa sasa ni mlemavu wa masikio, hajui akimbilie wapi ili asaidiwe kudai haki yake dhidi ya ukiukwaji huu a haki za binadamu.
Kijana Nuru Togwa (30) ambaye amekatwa masikio yake yote mawili, akiwa na mdogo wake aitwaye Sukuma Togwa nyumbani kwao katika kijiji cha Malonje nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga. |
No comments