Breaking News

MPANDA WAKABILIWA UHABA MKUBWA WA MAJI

Na Mwandishi wetu, Mpanda.
Mji wa Mpanda mkoani Katavi unakabiliwa na tatizo ukosefu huduma ya maji kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja sasa.
Hali hiyo imejitokeza kutokana na mamlaka ya maji taka na maji safi ya Halmashauri ya mji wa Mpanda  kukatiwa umeme na shirika la umeme baada ya kushindwa  kulipa bili ya umeme.
Kukosekana kwa maji kumesabisha ndoo moja kupanda kwa bei ambapo sasa inauzwa kati Sh 500 hadi 800 tofauti na awali ambapo ilikuwa ikiuzwa Sh 300.
Meneja wa mamlaka ya maji safi na maji taka wa mji wa Mpanda, Galus Kasonso alisema tatizo hilo limetokana na mamlaka ya maji taka na maji safi kushindwa kulipa bili ya umeme.
Alisema mji wa Mpanda unategemea maji yanayotoka katika bwawa la Milala na yanasukumwa na pampu ya mashine na wananchi wengine wanapata maji ya kutengwa yanayo toka kwenye mto Manga.

No comments