Breaking News

Watu nane wafariki dunia katika ajali ya gari mkoani Katavi

WATU nane wamefariki dunia papo hapo   na wengine kumi kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya baada ya  gari aina ya Fuso waliokuwa wakisafiri kuacha njia na kupinduka katika eneo la mlima  Katete uliopo katika Kijiji cha Milumba   Kata ya Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi

 Ajali hiyo  ambayo ililihusisha  fuso  lenye namba za usajiri    T 234 AXK  lilikuwa likiendeshwa na  Jamali Mohamed(42) Mkazi  wa   Mbagala Dares salaam  ilitokea  jana alfajiri ya saa 11  katika eneo la mlima  Katete  barabara itokayo Kibaoni wiayani Mlele kuelekea  Sumbawanga Mkoani Rukwa

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi aliwataja waliokufa kuwa ni  Peter Lusambo (24),Ngelela Shaulitanga (29),   John Pius(32) ,  Linus (30) aliyetambulika kwa jina moja   wote hao wakazi wa Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi

Kidavashari aliwataja waliokufa wengine kuwa ni  Makono  Kisumu (23) Elias Mussa(28) wakazi wa  wilaya ya Geita Mwanza  Ally (34) Mkazi wa Dares salaam ambae alikuwa utingo wa gari hilo na   Abasi (28) alitambulika kwa jina moja mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel Wilayani Mpanda

 Kamanda Kidavashari aliwataja majeruhi wa ajali hiyo ambao ni  Kaswagula  Linusi  25  Peter Mkalala 30 Peter Lusambo  20 Castory Kaombwe  23 Nassor  Ramadhan  22 wakazi wa Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi

 Wengine ni Salim Hassan  42  mkazi wa Mwanza  Jamari  Mohamed 42 Salumu  Njomoke  22 wakazi wa Dares salaam  John  Chambaneje  32  Mkazi wa  Mtaa wa Mpanda Hoteli  mjini  Mpanda

 Kamanda Kidavashari alisema  chanzo cha ajali  hiyo  ilitokana na  gari hilo  kukatika Propela  shafuti  hari iliyosababisha  gari kuacha njia na kupinduka ambapo majeruhi hao wote  wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda na wanaendelea kupatiwa  matibabu  na hali zao zinaendelea vizuri

 Kidavashari alieleza  dereva wa gari hilo  lililopata ajali  amekamatwa  na anatarajiwa  kufikishwa  mahakamani  mara baada ya upelelezi kukamilika

No comments