BASI LACHOMWA MOTO BURUNDI
Basi moja la uchukuzi limechomwa
moto mjini Bujumbura Burundi na waandamanaji waliorejea mabarabarani
kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Waandamanaji wanachoma moto magurudumu haswa katika eneo la Kanyosha.
Kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha maandamano haya dhidi ya awamu ya tatu ya rais Nkurunziza.
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Ismael Misigaro amesema milio ya risasi inasikika mjini humo. Maandamano
haya yanarejea baada ya kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani Zedi
Feruzi nje ya nyumba yake katika mji mkuu Bujumbura.
Aidha
wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha mazungumzo na serikali
rais Pierre Nkurunziza ya kutaka kutanzua mzozo ulioko wa kisiasa.
Mzozo huo unafuatia hatua ya Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu. Uamuzi
ambao wengi wanasema kuwa unaenda kinyume na sheria na ndio
iliyosababisha kuwepo kwa jaribio la kumpindua, na maandamano ya wiki
kadhaa. Tayari zaidi ya raia 100,000 wa taifa hilo wametorokea mataifa jirani.
SOURCE: BBC
No comments