MAMBO YAMEIVA CHADEMA S'WANGA, WAGOMBEA WAREJESHA FOMU.....Ngogo apania kumng'oa Malocha, Vita ni Upendo na Ikuwo
Mussa Mwangoka,
KIJANA Daniel Naftali Ngogo (28)amerejesha fomu hii leo kuomba kuteuliwa na Chadema ili awe mgombea ubunge katika jimbo la kwela lililopo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Ngogo alirejesha fomu yake leo katika ofisi za Chadema, ambapo akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa yeye amesukumwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kutokana na kukosa uwakilishi sahihi kwa muda mrefu sasa.
Ngogo (28) ambaye anaingia katika
kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo linaloongozwa na Ignas Malocha.
Alitaja vipaumbele vyake vitatu ambavyo akipata fursa hiyo atakwenda vifanyia kazi iwapo ataweza kuchaguliwa kuwa mbunge ambavyo ni Elimu, Afya, kuboresha miundombinu ya barabara na ajira jimboni kupitia kilimo.
Huyo anakuwa mtu wa pili kurejesha fomu yake ndani ya Chadema baada ya jana mfanyabiashara wa mjini Sumbawanga, Casiano Kaegele, maarufu kwa jina la Upendo ambaye alirudisha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea jimbo la Sumbawanga mjini ambalo kwa sasa linaoongozwa na Aeshi Hilaly.
Kaegele
akirejesha fomu alisema amesukumwa na mambo kadhaa kugombea ubunge
katika hilo yakiwemo ya kuanzisha miradi ya wajasiliamali kukabiliana na
tatizo la ajira kwa vijana na wanawake.
Pia kuboresha miundombinu ikiwemo ya kuhakikisha jimbo hilo linakuwa na kiwanja cha ndege hali ambayo itaondoa hadha ya wananchi kwenda mkoa wa jrani mbeya kwa ajili ya kupata huduma hiyo.
Kuingia katika kinyang'anyiro hicho kwa Upendo kunafanya kinyang'anyiro cha kumpata mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema kuwa kigumu kwani mfanyabiashara huyo mkubwa amekuwa na uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wananchi wengi akiwemo wanachama wa Chadema.
Lakini pia Sadriki Malila maarufu kwa jina la Ikuwo naye anadaiwa kuwania nafasi hiyo na anatajwa kuwa na wafuasi wengi wanaomuunga mkono katika harakati zake hizo.
KIJANA Daniel Naftali Ngogo (28)amerejesha fomu hii leo kuomba kuteuliwa na Chadema ili awe mgombea ubunge katika jimbo la kwela lililopo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Ngogo alirejesha fomu yake leo katika ofisi za Chadema, ambapo akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa yeye amesukumwa kugombea ubunge katika jimbo hilo kutokana na kukosa uwakilishi sahihi kwa muda mrefu sasa.
Katibu wa Chadema wilaya ya Sumbawanga mjini, Pius Nguvumali (kushoto) akipokea fomu kutoka kwa Daniel Ngogo (kulia) |
Alitaja vipaumbele vyake vitatu ambavyo akipata fursa hiyo atakwenda vifanyia kazi iwapo ataweza kuchaguliwa kuwa mbunge ambavyo ni Elimu, Afya, kuboresha miundombinu ya barabara na ajira jimboni kupitia kilimo.
Huyo anakuwa mtu wa pili kurejesha fomu yake ndani ya Chadema baada ya jana mfanyabiashara wa mjini Sumbawanga, Casiano Kaegele, maarufu kwa jina la Upendo ambaye alirudisha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea jimbo la Sumbawanga mjini ambalo kwa sasa linaoongozwa na Aeshi Hilaly.
Katibu wa Chadema wilaya ya Sumbawanga mjini, Pius Nguvumali, akipokea fomu kutoka kwa mfanyabiashara Casiano Kaegele |

No comments