KINYANG'ANYIRO CHA URAIS.....Membe amwagia sifa Pinda, asema kama sio yeye basi mtoto wa mkulima
Mussa Mwangoka,
Sumbawanga.
WAZIRI wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, ambaye
pia ni mgombea urais ndani ya CCM Bernad Membe amekiri kwamba katika kinyang’anyiro
cha urais ndani CCM mtu anayemnyima usingizi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Membe alisema kuwa iwapo Pinda asingechukua fomu ya urais
ndani ya CCM angekuwa anafurahia ushindi tu na tayari angekuwa ameshona suti na kushangilia ushindi.
alisema hayo jana kwenye ukumbi wa CCM Sabasaba wakati akizungumza na wadhamini wake waliojitokeza kwa wingi.
Alisema
kuwa Waziri Mkuu Pinda ni mtu mchapakazi,asiye mbinafsi, mwadilifu,
mvumilivu sana mwenye hekima na busara ya hali juu, mwanasheria
aliyebobea na ndiye mwalimu wake ambaye alimfundisha kazi.
"Wengine
wote hawanitishi nitawagonga nitawagonga lakini nikifika kwa Pinda
itabidi nipumue kwanza......kwa hiyo mimi na Pinda ni pacha nikishindwa
mimi nitamuunga mkono lakini akishindwa naamini ataniunga mkono, ndio
maana hata wakati nakuja huku nimewasiliana nae akinieleza nenda na
amenisaidia nimepata wadhamini wa kutosha" alisema.
Membe
amesema kuwa mungu akimjaalia kuteuliwa na CCM kushinda urais
atahakikisha baadhi ya miradi inayotumia fedha za ndani ambayo inasuasua
ikiwemo ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Mpanda unakamilika,
lakini pia bonde la Ziwa Rukwa linatumika kuzalisha chakula ambacho
kitalisha nchi nzima kwa kuwa ardhi yake ina rutuba na inafaa kwa
kilimo.
Pia, Membe
aliwaasa baadhi ya wanaccm kuacha kuwashangilia kila mgombea anayepita
kuomba udhamini kwa kuwa sio wote wana sifa kwani wenye sifa stahiki ni
yeye na Waziri mkuu Pinda.
Awali,
Katibu uenezi wa mkoa huo, Clement Bakali alisema kuwa mgombea huyo
amepata wadhamini 855 kutoka wilaya zote za mkoa wa Rukwa.
No comments