Breaking News

NYAMA YA KONGONI YAMPELEKA JELA MIAKA 20

MAHAKAMA ya  ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi imemuhukumu  kifungo cha miaka 20 jela Mkazi waMtaa wa Nsemlwa  Mjini Mpanda,  Emili Felix  baada ya kupatikanana  na kosa  la kukamatwa  akiwa   na kilo 120 za nyamaya Kongoni yenye thamani ya Sh 600,000 (laki sita)
Mshitakiwa alihukumiwa adhabu hiyo hapo juzi mbele  yaHakimu  mkazi  mfawidhi wa Mahakama ya Wilayaya MpandaChiganga Ntengwa  baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa  mahakamani hapo wa pande mbili za mashitaka na utetezi
 Awali  katika kesi hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria   wa   Hifadhi ya Taifa Katavi, Pele  Malima aliiambia Mahakama kuwa  mshitakiwa Emili alitenda kosa hilo Februari  12 mwaka 2011 majira  ya saa nne usiku
Ilidiwa  mahakamani hapo na mwendesha mashitaka huyo wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi  kuwa siku hiyo ya tukio  Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walipata taarifa  kutoka kwa raia wema kuwa  mshitakiwa amekuwa akijihusisha na uwindaji  haramu katika hifadhi ya Taifa ya Katavi, ndipo walipokwenda kumpekua nyumbani kwake na walifanikiwa kumkamata akiwa na kilo 120  za nyama ya Kongoni
Katika kesi hiyo  upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi wanne ambapo mshitakiwa  hakuwa nashahidi yoyote naalijitetea mwenyewe
KablayakusomahukumuhiyoHakimuChiganga  alimpa  nafasi  mshitakiwa ya  kuweza kujitetea  ilikama  anaweza kuwa  na sababu ya msingi inayoweza  kiishawishi  mahakama ipunguzie  adhabu  
Katika utetezi wake mshitakiwa  Emili aliomba  mahakama impunguzie adhabu  kwa kile alichodai kuwa     ana umri  mkubwa wa miaka 61  na kuna familia ambayo inamtegemea
Hata hivyo utetezi huo ulipingwa vikali  na   mwendesha mashitaka wa   Hifadhi ya Taifa ya Katavi  na aliiomba  mahakama itowe  adhabu kali kwa mshitakiwa  kwani tatizo la  kukamatwa kwa wawindaji  haramu  limekuwa likiongezeka siku hadi siku  hivyo  aliomba  mahakama itoe  adhabu  kali  ili iwe fundisho kwa wawindaji  haramu haramu
Akisoma  hukumu  hiyo   Hakimu   Chiganga  alieleza kuwa mshitakiwa  amepatikana  na  kosa  na kuvunja  sheria  ya kifungu  namba  86(1)  (2)  (c) (i) cha  sheria  ya wanyama  pori  namba 5 ya mwaka 2009
Hivyo   Mahakama  pasiposhaka  lolote imetowa adhabu  kwa  mshitakiwa    kutumikia jelakifungo cha miaka  ishirini kuanzia sasa.

No comments