WATU NANE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMKATA MKONO ALBINO MKOANI KATAVI
Walter Mguluchuma, Mpanda.
WATU wanane wamefikishwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi kujibu shitaka
la kumjeruhi kwa mapanga na kisha kumkata mkono na kutomomea nao wa mwanamke
mmoja aitwaye Remi Luchumi (30) mkazi wa Mwamachoma Tarafa
ya Mamba Wilaya ya Mlele na kisha kutokomea nao
Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani hapo
jana mbele ya Hakimu mkazi wa
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa
Katavi Odira Amworo
Washitakiwa hao nane waliopandishwa
kizimbani ni Alex Manyanza (24) Nogele Maliganya (Hombohombo) 40 Galula
Nkuba(45) Shile Jilala(27) Masunga
Kashinje(34) Maiku Punga (27) Koga Silanga(32) wote wakazi wa Kijiji cha Maji
moto Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele na
Salumu sawa Mkazi wa Meatu
Shinyanga
Mwendesha mashita
mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Hongera Mwakifimbo alidai mahakamani hapo kuwa, watuhumiwa
walitenda kosa hilo hapo Mei 14 mwaka huu nyakati za saa sita usiku nyumbani kwa wazazi
wake na Albino huyo katika Kijiji cha
Mwamachoma
Watuhumiwa
wanadaiwa kwamba siku hiyo ya tukio walikwenda
nyumbani kwao na Remi Luchoma
na walimkuta akiwa amelala na kisha walimjeruhi kwa mapanga sehemu ya
mkono wake na kisha walifanikiwa kumkata kingaja cha mkono wake na kisha walitokomea nacho
Baada ya kusomewa mashita na mwanasheria
wa serikali Mawiti Malifimbo katika kesi hiyo ambayo ilimevutia hisia za
watu wengi wa Mkoa wa Katavi
Washitakiwa wote kwa pamoja walikana
kutenda kosa hilo na waliomba Mahakama iwape dhamana kwa kuwa walikuwa na watu wa kuwadhani
Hata hivyo
maombi hayo yalipigwa vikali kwa kile kilichodaiwa na mwanasheria wa
Serikali kuwa endapo washitakiwa watapewa dhamana wanaweza kuharibu ushahidi
kwani bado kuna watuhumiwa wengine wanaendelea kutafutwa
Hakimu
Odira baada ya kusikiliza maombi
ya pande hizo mbili aliamuru washitakiwa
wapelekwe rumande hadi hapo Julai 15
ambapo kesi hiyo itakapo tajwa
tena
Tukio la kukatwa
kwa mkono kwa Albino huyo limekuwa ni la kwanza
kutokea katika Mkoa wa Katavi tangia
kuanza kutokea kwa mauaji ya
Albino hapa nchini
No comments