Watendaji wa Serikali waagizwa kuacha urasimu katika utoaji wa habari
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akifurahia picha ambayo inamuonyesha baba yake mzazi mzee Moses Nnauye alipiga na Mwanasiasa Mkongwe nchini Dr Chrisant Mzindakaya, baada ya kukabidhiwa picha hiyo jana na Dr Mzindakaya.
WAZIRI Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameagiza watendaji wa Serikali katika halmashauri za wilaya na mikoa nchini kuachana na urasimu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kwani kufanya hivyo kunanyima uhuru na haki ya wananchi kupata habari.
Alisema hayo jana mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, wakati akizungumza na wadau wa Sekta ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa huo (RDC) uliopo mjini hapa.
Nnauye alisema kwamba kumekuwapo na malalamiko kadhaa kutoka kwa wadau wa sekta ya habari kwamba baadhi ya taasisi za Serikali hususani halmashauri zimekuwa na urasimu katika utoaji wa taarifa kwa vyombo vya habari hali ambayo inafanya baadhi ya vyombo vya habari kutoripoti taarifa sahihi hivyo kuipotosha jamii.
"Tusiwalaumu waandishi au vyombo vya habari kwa kuandika taarifa za upotoshaji wakati wenye jukumu la kutoa taarifa sahihi ni nyie watendaji wa serikali,....sasa kama mnaficha habari maana yake mnataka watunge za kwao na kuzichapisha" alisema Waziri huyo.
Pia aliwaasa wanahabari kufanya kazi kwa weledi ili kutoruhusu baadhi ya watu wasiolitakia taifa mema kutumia mwanya huo kupenyeza sumu za udini, ukabila na ukanda kitu ambacho ni hatari na kinaweza kuligawa taifa.
Mmoja wa wadau wa habari, Sadric Malila aliitaka serikali kuangalia upya namna ya ulipaji ada za leseni kwani kwa sasa wamiliki wa vyombo vya habari hususani redio na Televisheni wanalipa kwa kutumia mfumo wa dola za kimarekani badala ya Shilingi ya kitanzania hali ambayo inafanya walipe fedha nyingi pindi shilingi inapoporomoka katika soko la fedha.
Kauli hiyo pia iliungwa mkono na Mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Chrisant Mzindakaya ambaye alidai kwamba serikali inawajibu wa kudhibiti matumizi ya dola hapa nchini hasa kwa wananchi wa kawaida.
Alisema imefika sasa sio tu biashara zinafanyika kwa dola lakini hata baadhi ya wamiliki wa nyumba wanapangisha nyumba zao wakitaka kulipwa kwa dola badala ya shilingi kitu ambacho ni mzigo kwa wananchi pindi mabadiliko ya kiuchumi yanatokea.

No comments