Walimu waandamana Mpanda, Viongozi wakimbia ofisi zao
Walter Mguluchuma, Mpanda.
Hali haikuwa shwari kwa zaidi ya saa
moja kwenye Ofisi za Manispaa Halmashauri ya
Mpanda, jengo ambalo linatumiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi baada ya waalimu zaidi ya 50 washule za
Msingi na Sekondari wakiwa na viongozi kuandamana
kwenda kwa mwajiri wao wakitaka walipwe ya madai ya Sh milioni 120.
Tukio hilo liltokea jana nyakati
za saa nne asubuhi, hali ambayo ilisababisha viongozi
wa Manispaa hiyo kuweza kujifisha huku walimu hao wakiimba
nyimbo mbalimbali kwenye kolido za ofisi hizo kwa saa moja na zaidi.
Hali hiyo iliwalazimu viongozi wa mkoa na Manispaa hiyo
kujitokeza na kufanya kikao cha dharula na walimu hao waliokuwa wameambatana na
viongozi wa Chama cha walimu (CWT) wilaya na mkoa.
Kaimu katibu tawala wa Mkoa
huo, Salumu Shilingi ndiye aliyejitosa kusikiliza kilio
hicho cha walimu, huku CWT wakiongozwa na katibu wa
mkoa, John Mshota ambaye aliwasilisha madai
mbalimbali ya walimu hao ambayo yamekuwa sugu.
Mshota aliyataja madai hayo kuwa kucheleweshewa kurekebishiwa mishahara,
kutolipwa fedha za
nauli za likizo kuanzia mwaka 2013
hadi 2015, kutolipwa gharama
za masomoni, kutolipwa kwa
walimu wastaafu za kuwarudisha kwao,gharama za
uhamisho na fedha za matibabu.
Mwenyekiti huyo wa CWT Mkoa
wa Katavi alieleza kuwa mwajiri
wao ambaye ni mkurugenzi
wa Manispaa ya Mpanda, ameshindwa
kupeleka michango wake kwenye
mfuko wa PSPF hali ambayo imewaathiri walimu wanaostaafu kutolipwa
malipo yao ya mafao ya kinunua mgongo kidogo na
kutopewa hati zao za malipo yao ya msharahara
Salary Slips za mwezi Agosti 2008.
Alisema kutokana na madai
hayo, ndio maana waliamua kuandamana hadi
ofisini kwa mwajiri ili waweze
kupatiwa majibu ya madai yao wanayodai
kwa muda mrefu sasa bila
kuwepo dalili za kulipwa madai hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, ambaye ni Ofisa Elimu Sekondari,
Enelia Lungulu alikiri mbele
ya walimu hao kuwepo kwa madai hayo ya walimu.
Aliongeza kwamba tatizo
la kutolipwa kwa walimu hao halipo
kwao bali tatizo la kucheleweshewa kwa malipo hayo
lipo hazina ambayo mpaka
sasa hawazituma fedha za madai ya
walimu kwenye Manispaa hiyo na jitihada za
mawasiliano zinaendelea kufanyika.
Serikali iwalipe walimu iache longolongo mbona madeni mengine inalipa kwanini walimu tu?.
ReplyDeleteSerikali iwalipe walimu iache longolongo mbona madeni mengine inalipa kwanini walimu tu?.
ReplyDelete