Breaking News

Wazazi Nkasi lawamani kwa kutokomesha mimba za utotoni

Wadau wanaounda timu ya Ulinzi wa watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni wakifuatilia mada katika kikao cha robo mwaka cha timu hiyo.

Wazazi na walezi wilayani Nkasi mkoani Rukwa, wametakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola, ili iwe chachu ya kupunguza mimba za utotoni wilayani humo.


Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya, Ramadhani Rugemalila alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha robo mwaka cha timu ya ulinzi dhidi mimba na ndoa za utotoni, kilichoandaliwa na Shirika la Plan International linalotekeleza mradi wa kuzuia mimba za utotoni chini ya ufadhili wa NORAD.

Alisema kuwa kumekuwa na kasumba iliyojengeka miongoni mwa wazazi na walezi ya kuripoti matukio ya mimba kwa watoto wao wa kike katika vituo vya polisi, lakini mashauri yanafikishwa mahakamani wamekuwa wakikacha kufika ili kutoa ushahidi.

Alisema kutokana na hali hiyo mashauri hayo yamekuwa yakiondolewa mahakamani kwa kuwa hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani watuhumiwa ndipo wazazi hao uibuka na kuitupia lawama mahakama kwa hakutenda haki.

Mwalimu wa shule ya Sekondari, Mkwamba wilayani Nkasi, Adamu John akichangia mada katika kikao cha robo mwaka cha timu ya ulinzi dhidi mimba na ndoa za utotoni.

Wazazi na walezi badilikeni kifikra na mitizamo....mkitoa taarifa polisi za kesi za mimba sio kwamba ndio mmemaliza kila kitu ikihitajika kufika mahakamani kutoa ushahidi fikeni ili ushahidi mtakaotoa ndio utathibitisha kama watuhumiwa wana hatia au la ili sheria ichukue mkondo wake" alisema Rugemalila

Alisema tofauti na hivyo msilalamike pindi shauri linapoondolewa mahakamani kwa kukosekana kwa ushahidi wa walalamikaji.

Aidha, takwimu kipindi cha mwaka mmoja uliopita zinaonyesha wilaya hiyo ilikuwa na mimba hizo 53 ambapo sekondari ni mimba 33 na msingi ni wanafunzi 20 wa shule za msingi walipewa ujauzito. 

Naye, Mratibu wa mradi huo, Nestory Frank mradi huo unaotekelezwa katika kata tatu za mfano ambazo ni Mtenga, Nkandasi na Mkwamba umebaini tatizo la mimba na ndoa za utotoni ni kubwa kwa zaidi ya asilimia 50 ambapo watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wana ujauzito na wengine wamezaa wakiwa nyumbani.

Alisema baada ya kubaini tatizo hilo, Shirika la Plan International kwa kushirikiana na chuo cha maendeleo ya jamii ya Wananchi cha tarafa ya Chala walianza kutekeleza mradi kuwawezesha vijana hao kiuchumi kupitia mpango wa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi.
Wadau wanaounda timu ya Ulinzi wa watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni wakifuatilia mada katika kikao cha robo mwaka cha timu hiyo.

Alisema licha kuwapatia elimu hiyo lakini kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watoto wa kike kukacha mfunzo hayo kwa madai wao ni warembo na hawezi kufanya kazi ya ufundi hivyo kukimbilia maeneo ya mjini ili kufanya shughuli za kuuza vinjwaji baa.

Inadaiwa watoto wa kike kike 22 kati ya 70 wamekimbia mafunzo katika kata ya Nkandasi na Katani, ambapo hatua zilizochukuliwa hivi sasa ni kuhakikisha kamati za usimamizi wa vituo hivyo katika kila kijiji zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto hao.

No comments