Breaking News

Vitanda vya wajawazito bado changamo Rukwa.


Mwandishi wetu, Rukwa.

Wakinamama wajawazito mkoani Rukwa wanalazimika kujifungulia sakafuni kutokana na vituo vingi vya afya kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vitanda, imefahamika.

Mjumbe wa bodi ya shirika lisilo la kiserikali la uhamasishaji  uchangiaji damu liitwalo Association of Rare Blood Donor (ARBD), Bathromeo Mwanansya alisema hayo jana wakati akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vitanda na magodoro  55 vyenye thamani ya Sh milioni 47 vilivyotolewa na SHirika hilo.

Alisema kuwa shirika lao limefanya utafiti katika baadhi ya vituo vinavyotoa huduma ya afya katika mkoa huo, na kubaini kwamba mahitaji makubwa ya ya vitanda kwa kuwa baadhi ya wagonjwa ulazimika kujifungulia sakafuni kutokana vituo vyao kukabiliwa na changamoto hiyo.  

Alisema kutokana na hali hiyo walilazimika kutafuta ufadhili kutoka nchini Marekani ambapo walipata fedha za kununua vitanda 20 vya kujifungulia wajawazito na 35 kwa ajili ya wagonjwa wa kawaida ambavyo vitagawiwa katika wilaya zote za mkoa huo.

Awali, Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa, Bonifas Kasululu alisema kuwa mkoa mzima unauhitaji wa vitanda 1,008 na vilivyopo ni vitanda 564 huku upungufu ni 444 sawa na asilimia 44.

Alisema kuwa msaada huo umetolewa wakati muafaka kwani vitasaidia kupunguza mahitaji yaliyopo ya vitanda na vifaa tiba vingine, ambapo aliwaomba wadau wengine kuiga mfano wa tasisi ya ARDB katika kuboresha huduma za afya mkoani humo.

Akipokea msaada huo, Mkoa wa Rukwa Joachimu Wangabo aliishukuru taasisi hiyo kwa msaada huo kwani imefanya kinacho stahili ambapo aliwakata wanawake mkoani humo kuwa na tabia ya kuhudhuria Kliniki na kujifungulia katika maeneo yanayotoa huduma za afya ili waweze kuwa salama wao na watoto wao wakati na baada ya kujifungua.

Alisema changamoto ya kupunguza vifo vya wajawazito inawezekana iwapo wakinamama hao watabadilika na kujenga utamaduni wa kujifungulia katika vituo vya afya badala ya majumbani na kwa wakunga wa jadi kama wanavyofanya baadhi yao.

Takwimu zinaonyesha kuwa mkoa wa Rukwa, una  vifo 117 vya wajawazito kati ya vizazi hai laki moja wakati takwimu za kitaifa ni vifo 506.

Mwisho

No comments