Breaking News

Mauaji ya kikatili Sumbawanga, kijana achinjwa watu watoweka na kichwa chake

     TUNAOMBA RADHI WASOMAJI WETU KWA PICHA HIZI ZA KUTISHA.

MATUKIO ya mauaji ya kikatili yameendelea kushamiri mkoani Rukwa, baada ya watu wasiojulikana kumuua kikatili mtu mmoja kwa kumchinja  na kutokomea kusikojulikana na kichwa cha mtu huyo.

Mwili wa mtu aliyeuawa kikatili kwa kukatwa kichwa ukiwa katika gari la polisi baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga leo asubuhi kwa ajili ya kuhifadhiwa. 

 Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio mtu huyo alifanyiwa unyama huo nyakati za usiku wa kuamkia leo ambapo mwili wa mtu huyo ulitupwa kando ya daraja la mto katusa ambako pembeni yake kuna makaburi katika mtaa wa Tambazi katika Manispaa ya Sumbawanga.

 Mwenyekiti wa mtaa wa Tambazi, Christopher Kwimba alisema kuwa mtu huyo aliyeuawa anakadiriwa kuwa na umri katika ya miaka 25 na 27 hivyo ni vigumu kumtambua kwa haraka kutokana na wauaji kuondoka na kichwa chake.

Baadhi ya askari polisi wakitelemsha maiti ya mtu ambaye ameuawa  kwa kukatwa kichwa na watu kutoweka na kichwa chake usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuhifadhi katika hchumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga.
facebook.comMwenyekiti huyo aliongeza kuwa watu hao baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kumtupa kwenye eneo hilo ambapo asubuhi ya kuamkia leo ndio kiwiliwili chake kilibainika kuwepo hapo lakini hakina kichwa kwani waliondoka nacho.

Kwa upande wake, Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa polisi inaendelea kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo hili hatua ziweze kuchukuliwa.

No comments