Mbunge S'wanga anadi fursa za uwekezaji za mkoa wa Rukwa nchini Burundi
Mbunge akimnong'oneza Mhariri wa Blogu ya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Bw. Hamza Temba, juu ya ziara yake fupi nchini Burundi. Alisema kuwa ziara yake hiyo nchini Burundi ilikuwa ya kikazi iliyomfanya ashindwe hata kuhudhuria Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania lililowasilishwa na Jamii za WanaRukwa na Katavi katika kijiji cha Makumbusho tarehe 15-17/11/2011.
Jambo muhimu na la msingi alioileza blogu hiyo ni juu ya mafanikio ya ziara yake hiyo kuwa aliapata fursa ya kukutana na baadhi ya Viongozi wa Serikali nchini Burundi akiwepo Meya wa Jiji la Bujumbura pamojana Wafanyabiashara wakubwa na kuwaeleza juu Fursa zinazopatikana Mkoani Rukwa.
Alisema kuwa wote walifarijika na kuonyesha nia ya kutembea na kuwekeza Rukwa. "Nimechukua contact zao na nitakachokifanya ni kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa ili kuwapa mualiko rasmi wadau hao waweze
kuja kutembea Rukwa na kujionea fursa zilizopo" alisema Mhe. Aeshi. Picha kwa Hisani ya Blog ya Mkoa wa Rukwa.



No comments