Breaking News

UDINI NA UKABILA UKEMEWE KWA NGUVU ZOTE KUNUSURU AMANI NCHINI.


Baadhi ya wazee wa manispaa ya Sumbawanga, kutoka kushoto ni  Mwl. Mstaafu Boniveture Mzurikwao na Raymond Sonjolo wakitoa ufafanuzi w jambo wakati wakizungumza na mwandishi blog hii. picha na Peti Siyame.

TANZANIA itaendelea kutajwa kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu iwapo  ukabila na udini unaoanza kujitokeza  utakemewa kwa nguvu zote.

Baadhi ya wazee wa Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, wamesema hayo leo wakati wakizungumza na mwandishi wa blog hii katika mahojiano maalumu yaliyofanyika  leo kwenye ofisi za chama cha wafanyabiashara wa viwanda na wakulima zilizopo mjini hapa. 

Mmoja wa wazee hao, Mwl. Mstaafu Boniveture Mzurikwao, alisema kuwa  udini na ukabila ukikemewa kwa nguvu zote taifa lipata mafanikio makubwa zaidi tofauti na haya yalipo hivi sasa  lakini tofauti hivyo amani itatoweka katika michache ijayo kuanzia sasa.

“watawala wasifumbie macho ukabila na udini unaoanza kuchipua……. Wakemee kwa nguvu zote kwani athari zake ni kubwa na amani na utulivu uliopo nchini utatoweka” alisema Mwl. Mzurikwao.

Naye Mzee Raymond Sonjolo, aliongeza kuwa tatizo jingine lililopo ni  tofauti kuwa ya walionacho na wasionacho ambayo athari zake ni watu kukata tamaa na kuanzisha vurugu hivyo sasa serikali inapaswa ilitafutie ufumbuzi suala tatizo hilo haraka iwezekanavyo.

Sonjolo alisema kuwa rasilimali na maliasili zilizopo zikitumika vizuri zitasaidia kuifanya nchi ipae kiuchumi lakini zikiendelea kutumika kwa manufaa ya watu wachache ni hatari kwa maendeleo ya taifa.

No comments