MKUU WA MKOA KUPAMBANA NA WANAOHUJUMU UJENZI WA BARABARA ZA LAMI RUKWA
| Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya. |
MKUU wa Mkoa wa Rukwa , Stella Manyanya ameonya kuwa hatasita kuwachukulia hatua za Kisheria
wale wote wataobainika kuhujumu mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga – Laela – Tuduma kwa kuiba vifaa vya ujenzi na mafuta mali ya makumpuni yanayojenga barabra hiyo kwa kiwango cha lami .
Alisema amelazimika kutoa onyo hilo katika kikao kilichofanyika jana mjini hapa ambapo kiliwajumuisha vinogozi waandamizi wa Serikali mkoani hapa , Wakandarasi wa mradi huo wa barabara , wawakilishilishi wa Shirika za Changamoto za Milenia (MCC-T) wakiongozwa na Mwakilishi wa Changamoto za Milenia kutoa Washngton DC , Jonathan Saiger
Mkuu huyo wa Mkoa pia aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani hapa kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya haki ili sheria ichukue mkondo wake .
Mhandishi Mkazi Paulo Grumette kutoka Kampuni la Kihandisi la Egis linalosimamisha mradi huo mkubwa wa barabara alifichukuwa kuwepo kwa genge la kiharifu ambalo alidai limesababisha kupungua kwa kazi ya ujenzi wa mradi huo kutokana kufanya wizi mkubwa wa vifaa vya ujenzi na mafuta
Alidai kuwa imebainika kuwa genge hilo la kihalifu likifadhiliwa na watu wanaodaiwa kutoka Jijini Dar Es Salaam na Mji wa Tuduma ulipo katika mpaka wa nchi jirni ya Zambia umeweza kuiba nondo zaidi ya tani 300 na saruji zaidi ya tani 40 na kuviuza nchi jirani ya Zambia .
Alisema kuwa genge hilo la kihalifu linawahusisha wakazi wa maeneo unapopita mradi huo wa barabara kwa kuwapa ajira ya muda ili kuwasaidia na kufanikisha wizi huo mkubwa ambao alidai ni vigumu kufanywa na wanavijiji pekee.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Manyanya aliwahakikishia wakandarasi hao kuwa Serikali mkoa kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinadhibiti wizi huo ambao kwa sasa umefikia hatua ya kutisha ili kuhakikisha kuwa mradi huo una malizika kama ulivyopangwa .
“ Tumesikia taarifa za wizi huo tena wa kiwango kikubwa sisi kama Serikali nawahakikishia kuwa tutaudhibiti ikiwa ni mchango wetu kwenu kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa pia nachukua nafasi hii kuwaaagiza watendaji wangu watembelee maeneo hayo na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa mradi huo “ alisem Manyanya .
Ujenzi wa barabara ya kutoka Tunduma – Laela – Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 225 kwa kiwango cha lami unafanya na makandarasi watatu tofauti kutoka China , Uturuki na Uholanzi ambapo lili kuharakisha ujenzi wake mradi huo umegawanya katika vipande vitatu vya Tunduma – Ikana , Ikana –Laela na Lela - Sumbawanga
Mradi huo ambao unatarajia kutumua zadi ya Sh bilioni 400 hadi utakapo kamilika unafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC).


No comments