Breaking News

TRA RUKWA, YATOA MSAADA KWA WENYE MAHITAJI MBALIMBALI.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Rukwa, Augustino Mkandara. Picha kutoka Maktaba. habari zaidi soma hapo chini.

MAMLAKA Kodi   ya  Mapato  nchini (TRA),  mkoani  Rukwa  imetoa   misaada    wagonjwa  waliolazwa  hospitalini  na   kwa  vituo   vinanvyosaidia  watoto  yatima  mkoani  humo

Vituo   viwili   vinavyosaidia  watoto   yatima  katika  mjini  wa  Sumbawanga   na  kingine  kilichopo   katika  kijiji  cha  kipande  wilayani  Nkasi,   kwa  pamoja  vikiwa   vinasaidia watoto   zaidi ya  sabini  na   wagonjwa  wa   hospitali  ya   mkoa   na   ile  ya  Dk.  Atman  zilizopo  mijini  humo. Walifaidika  na   misaada   hiyo

Kampuni  hiyo  , TRA  ilitoa   misaada ya    vyakula  vikiwemo   unga ,  mchele  pamoaja  na  sabuni  mafuta   ya  kupikia ,  premende   na  piskuti  vyenye   jumla  ya   zaidi  ya Sh 640,000=.

Akizungumza   kwa  nyakati  na   maeneo   tofauti   wakati   akitoa  misaada  hiyo  Meneja   wa  Mamlaka Kodi  ya  Mapato  mkoani  humo , Agustino  Mkandala   alisema TRA  imeamua  kutoa  misaada  hiyo  kama  sehemu  yake  ya  kujali  jamii

TRA ni  Mamlaka  ambayo  ina  mikakati  ya  kusaidia  jamii  kila   mwaka   kwa  kipindi  cha   miaka  mitano  iliyopita ……. Ndio  maana  tumeamua  kutoa  misaada  hii   kwa   vituo   vinavyosaidia  watoto   yatima   na  wagonjwa  mahospitalini

Huu  ni  utaratibu  ambao   TRA   imejiwekea   kwa   kipindi  cha  miaka    mitano  iliyopita  ambao  tunaenerdelea  nao  kila  mwaka “  alisema  Mkandala

Alifafanua kuwa  mkakati   huo  wa  kugawa misaada  kwa  makundi  yenye  mahitaji  maalumu  ni  sehemu  ya  maadhimisho  ya   wiki   mlipa  kodi  nchini   ambapo   inaadhimishwa  nchini   nzima na  kilele  chake  kitakuwa  Jumanne  wiki   ijayo .

Akizungumza  wakati  akipokea   msaada  hiyo  kwa niaba   ya  wafanyakazi    wa Hospitali  ya  Mkoa  iliyopo   mjini  hapa  Kaimu  Mganga  Mkuu wa Hospitali  hiyo, Dk  Sharack  Mtulla,  alisema   kuwa  wamefarijika  na  msaada  huo  ambapo  umekuja  wakati  muafaka  na  akashauri  misaada  ya jinsi   hiyo  iwe   endelevu

“ Tumefarijika  sana  tunaomba misaada hii   iwe endelevu   kwetu  ni  sehemu ya  tiba  kwa wagonjwa  wetu hapa   pia  naomba  taasisi  nyingine  pia  ziinge  mfano  wenu  kwani  kwa  hakika  mahitaji  tulionayo  katika  kuwahudumiwa  wagonjwa wetu  ni  mengi  pekee  yetu  hatuwezi “  alisema Dk Mtulla

Mwisho

No comments