Breaking News

POLISI JAMII YAREJESHA NIDHAMU KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI RUKWA

Jengo la polisi mkoa wa Rukwa.
MFUMO wa Polisi jamii na ulinzi shirikishi unaoendeshwa na Jeshi la polisi nchini, umeanza kupata mafanikio mkoani Rukwa baada ya kurejesha nidhamu ya baadhi ya wanafunzi wa Shule za sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Wanafunzi hao ni wa shule za Sekondari za serikali za  Kantalamba na Mafulala ambao walikuwa watoro kupindukia na kutumia muda wa vipindi vya darasani kunywa pombe za kienyeji aina ya ulanzi na kuvuta madawa ya kulevya aina ya bangi.

Mkuu wa kitengo cha Polisi jamii katika Jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa, Sixmound Kibasa, alisema wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha wadau wa habari kilichofanyika kwenye ukumbi wa RDC iliopo jengo la mkuu wa mkoa wa Rukwa, Kikao hicho kiliandaliwa juzi na Klabu ya waandishi wa habari wa mkoa huo (RKPC).

 Alisema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwapo kwa wanafunzi ambao wakitumia muda wa masomo kufanya vitendo hivyo viou sambamba na kunywa pombe walianza harakati za kuwatafuta na kuwapa somo la athari ya utoro, ulevi wa pombe na madawa ya kulevya.

"tuanzia Shule ya Sekondari ya wavulana ya Kantalamba tukawaeleza kwa lugha laini juu ya manufaa ya elimu kwao na kwa jamii nzima, athari za vilevi wanavyotumia.............
wakatuelewa, baada ya hapo tukaenda Sekondari ya Mafulala iliyopo kata ya Izia nako kulikuwa na tatizo kama hilo tukatoa elimu..... tunashukuru sasa wale vijana wamerejea shuleni na wana nidhamu ya hali ya juu" alisema Kibasa.
BAADHI ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakicheza kamali
kwenye moja vichochoro vya mtaa wa maendeleo mjini Sumbawanga, muda
ambao walitakiwa kuwa shuleni.

No comments