| | | MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya ameonya kuwa hatasita kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika kuhujumu mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya Sumbawanga – Laela mpaka Tuduma kwa kuiba vifaa vya ujenzi.
Ametoa onyo hilo jana alipotembelea kambi ya Ujenzi ya Mkandarasi Aarslef iliyopo kijijini Ikanda wilayani Sumbawanga ambao wanajenga kipande cha barabara kutoka Laela hadi Sumbawanga mjini kwa kiwango cha lami .
Alisema kuwa amelazimika kutoa onyo hilo kali kufuatia kwa taarifa ya wizi mkubwa wa vifaa vya ujenzi vikiwemo maelufu ya tani ya saruji , nondo na maelfu ya lita ya mafuta hususani mafuta ya dizeli vyote vikiwa mali ya kampuni hiyo ya ujenzi .
Pia aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani hapa kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.
Meneja wa Mradi wa Kampuni hiyo ya ujenzi , inayosimamia mradi huo, alidai kuna
genge la wahalifu ambalo alidai limesababisha kupungua kwa kasi ya ujenzi wa mradi huo kutokana kufanya wizi mkubwa wa vifaa vya ujenzi na ambapo zaidi ya lita 30,000 za mafuta ya dizeli zimeripotiwa kuibiwa .
Hivi karibuni akihojiwa na gazeti hili mjini Sumbawanga , Mhandishi Mkazi, Paulo Grumette kutoka Kampuni Egis inayosimamia mradi huo wa ujenzi wa barabara ya kutoka Tunduma - Laela - Sumbawanga kwa kiwango cha lami , alikiri kuwepo kwa genge la wahalifu ambalo alidai limesababisha kupungua kwa kasi ya ujenzi wa mradi huo kutokana kufanya wizi mkubwa wa vifaa vya ujenzi na mafuta.
Alidai kuwa genge hilo linafadhiliwa na watu wanaodaiwa kutoka jijini Dar ss Salaam na katika Mji wa Tuduma ulipo katika mpaka wa nchi jirani ya Zambia.
Kwa mujibu wa madai ya Grumette, genge limeshaiba nondo zaidi ya tani 300 na saruji zaidi ya tani 40 na kuviuza nchi jirani ya Zambia .
“Hali ni mbaya sana kwa kipande kile cha barabara kinachotoka Tunduma hadi Ikana, huko ndiko hujuma hiyo ya wizi mkubwa wa vifaa hivyo vya ujenzi na mafuta vinafanywa na
genge hilo la waahalifu,” alisema Grumette.
Alidai kwani eneo hilo limekubuhu kwa vitendo hivyo kwa kuwa ni rahisi kuvusha mali hiyo ya wizi na kuiuza nchi jirani ya Zambia.
|
| |
No comments