Watumishi wa Hospitali ya mkoa walivyoaga mwaka 2011 na kukaribisha mwaka 2012 jana usiku mjini Sumbawanga.
WATUMISHI wa Hospitali ya mkoa iliyopo mjini Sumbawanga, wametakiwa kuacha tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa kwani kufanya hivyo ni kujidhalilisha wao wenyewe na taaluma zao.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Abdul Maulid, alisema hayo jana wakati wa hafla ya kuuga mwaka jana 2011 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2012, iliyofanyika katika ukumbi wa hospitali hiyo uliopo mjini hapa.
Alisema kuwa ni aibu na kujidhalilisha kwa watumishi hao kuomba rushwa kutoka kwa wagonjwa wanaofika hospilini hapo kwaajili ya kupata matibabu hali ambayo inasababisha wagonjwa hao kupoteza imani nao hivyo watumishi hao kudharaulika wao na taaluma zao katika jamii.
"nawasihi mfuate maadili ya kazi yenu.....msiwe walevi kupindukia na msipokee rushwa kutoka kwa wagonjwa kwani kufanya hivyo ni kujifedhehesha..... tuikatae rushwa, tena rushwa ndogo ndogo ni mbaya na udhalilishaji mkubwa kwa taaluma yenu" alisema Kaimu Mkurugenzi huyo ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya katika hafla hiyo.
Naye, Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa, Dk. Shadrack Mtulla aliwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kadri ya uwezo wao licha ya kuwapo kwa changamoto nyingi ambazo zinawakabili ikiwamo ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa.
 |
No comments