Breaking News

ROTARY CLUB YATOA ZAWADI MBALIMBALI KWA WATOTO YATIMA S'WANGA.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akimvalisha "gloves" mtoto Juma Kapela ambaye ni mlemavu wa ngozi (Albino) jana muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na Rotary klabu ya Sumbawanga kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Katandala kilichopo chini ya kanisa katoliki jimbo la Sumbawanga.
Rais wa Rotary Klabu ya Sumbawanga, Reina Lukara akitoa taarifa fupi jana kwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kulia wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto yatima wanaolelea katika kituo cha Katandala kilichopo mjini Sumbawanga, kushoto kwake ni Askofu wa Maiko Badeleya wa kanisa la Anglikana.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya, akimkabidhi mkuu wa idara ya afya jimbo katoliki Sumbawanga, Sister Helena Katebela  zawadi mbalimbali zikiwamo na vyandarua  zilizotolewa na Rotary klabu ya Sumbawanga kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Katandala kilichopo chini ya kanisa katoliki jimbo hilo. 

No comments