Kiboko azua tafrani kijijini.....asababisha wananchi washinde kutwa nzima mitini.
Na Walter Nguluchuma, Katavi.
BAADHI ya wakazi wa Kitongoji cha Kashalami Kata ya
Mashimboni wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelazimika kushinda juu ya
miti kwa kuhofia kushambuliwa na Kiboko aliyevamia kijiji hicho na
kuhatarisha uhai wao.
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo ya Mashimboni, Raphael
Kalinga, tukio hilo lilitokea hapo Agos 18 nyakati za saa moja na nusu
asubuhi
Akielezea tukio hilo alisema Kiboko huyo baada ya kuvamia
kijiji hicho alielekea kwenye nyumba ya mkazi mmoja aitwaye Joseph
Kashamakula ambae alinusurika kushambuliwa na Biboko huyo wakati
alipokuwa akitokea chooni kujisaidia
Diwani Kalinga, alisema ndipo Kiboko huyo ambae
alionekana kuwa na hasira alipoanza kukanyaga kanyanga na vuvivunja
vyombo vya mwanakijiji huyo ambavyo vilikuwa nje ya nyumba yake na
kuviharibu kabisa hali ambayo ilimfanya wananchi huyo apige mayowe ya
kuomba msaada kwa majirani
Majirani walifika kwenye eneo hilo hata hivyo
walilazimika kutimua mbio baada ya kiboko huyo kuanza kuwafuata
hali ambayo ilisababisha kukimbia na kisha kupanda juu ya miti kwa
kuhofia kushambuliwa na mnyama huyo ambae aliendelea kuvunja vyombo
kwenye nyumba mbalimbali
Alisema kuwa kiboko huyo aliendelea kuharbu vitu kwenye
eneo la kijiji hicho na taarifa za zilifika kwenye Idara ya Maliasili
ya Halmashauri ya Nsimbo ambao walituma askari wao wa wanyama pori
kwenda huko
Baada ya askari wa Maliasli kufika kijijini hapo walianza
msako wa kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi ambapo walifanikiwa
kumwona na kisha walimuua kwa kumpiga Risasi tumboni na kichwani
Diwani Kalinga alieleza baada ya Kiboko kuuawa
wananchi licha ya hapo awali kumkimbia kiboko huyo walianza kugombea
nyama ya mnyama huyo kwa kuchukua kitoweo cha mboga na baada ya
nusu saa wakawa wamemmaliza.
No comments